Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Profiles Cheo

Hon. William Tate Olenasha

Utumishi:
2015 - 2020 (Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi)

Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1972-05-27
Mahali pa Kuzaliwa: Kakessio, Ngorongoro- Arusha

Ndoa: AmeoaMaelezo


Mhe. William Tate Olenasha ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alizaliwa Mei 27, 1972 katika kijiji cha Kakessio wilaya Ngorongoro mkoani Arusha.

Elimu.

Alianza Elimu ya Msingi mwaka  katika shule ya Msingi Kakessio mwaka 1978 na kuhitimu mwaka 1984. Kisha aliendelea na Elimu ya Sekondari katika Seminari ya Kanisa Katoliki Arusha mwaka 1986 hadi 1989. Aliendelea na Masomo ya Elimu ya Sekondari kidato cha Tano na Sita katika shule hiyo hiyo mwaka 1990 hadi 1992.

Mara baada ya kuhitimu masomo ya Elimu ya Sekondari Mhe. Olenasha alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 1996 hadi 1996 kusomea Shahada ya Sheria (LLB). Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, mwaka 2000 alijiunga na Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika ya Kusini kusomea Shahada ya Umahiri katika Sheria (LLM) ambayo alihitimu mwaka 2001. Pia  alihitimu ngazi ya Cheti katika Utawala Bora mwaka 2000 na Cheti  cha Masuala ya Haki za Binadamu katika Chuo Kikuu cha Pretoria.

Uzoefu Kazini.

Kitaaluma Mhe. Olenasha ni Mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu. Aidha, baada ya kuhitimu Shahada ya kwanza aliajiriwa na kampuni ya uwakili ya FK Law Chambers iliyoko jijini Dar es salaam.Kati ya mwaka 2002 hadi 2005 Mhe. Olenasha mara baada kurejea nchini Tanzania akitokea nchini Afrika ya Kusini aliajiriwa na Jukwaa la Taasisi za Wafugaji kama Ofisa wa Programu na Mchambuzi wa Sera. Mwaka 2005 hadi 2009 aliajiriwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam akiwa mtaalam wa Ardhi na Ufugaji wadhifa ambao ulimsaidia kujifunza namna nchi nyingine zinavyonufaika na kuwekeza kwenye ufugaji na kutengeneza miundombinu bora ya ufugaji.

Mwaka 2010 hadi 2011 alifanya kazi akiwa mratibu na mshauri mtalaam wa kimataifa katika Mradi wa Kimataifa uitwao Ascertainment of Customary Law Project uliodhaminiwa na Wizara ya Sheria ya Serikali ya Sudani Kusini ikishirikiana na Shirika la Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Aidha, Mhe. Olenasha mbali na majukumu hayo, toka mwaka 2012 hadi sasa ni Wakili wa kujitegemea, mwanachama wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika Law Society) na kile cha Afrika Mashariki (East Africa Law Society). Pia mwaka 2014 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Pia Mhe. Olenasha amewahi kufanya kazi na Shirika la Kimataifa la Care International katika Mradi maalum uliohusisha mashirika yenye maslahi mapana kwenye Ardhi na ambayo yana ushawishi katika utungaji wa Sera za Ardhi hapa Tanzania.

Pia amewahi kupewa kazi ya kuunda mfumo wa kufuatilia uwekezaji katika Ardhi katika nchi zilizoko katika jangwa la Sahara kwa kutumia uzoefu wa Tanzania, Kazi hii alipewa na kuifanya mwaka 2012 na taasisi ya IIED ikishirikiana na Taasisi ya Melinda na Gates. Pia mwaka 2011 Kituo cha Haki za Binadamu na Sheria cha nchini Uganda kilimpa kazi kuandika taarifa ya kina juu ya maendeleo na mchakato wa Katiba wa Tanzania.

Machapisho Mbalimbali.

Mhe. Olenasha ameandika machapisho mbalimbali yakiwemo “Legal Tools for Citizen Empowerment, ED, 2013” , chapisho lijulikanalo kama  “Reforming Land in Tanzania for whose Benefit, 2004 ‘’ pia chapisho lijulikanalo  kama “The Case of Ethnic and Racial  Minorities in Tanzania” , Kituo cha Katiba, 2009. Pia ameandika chapisho kuhusu Urithi wa Ngorongoro “ A World Heritage in Ngorongoro ,Whose World, whose Heritage , 2015  na lile la Parks without People : The Case of Ngorongoro Conservation Area, 2006.

Nishani na Tuzo.

Mhe. Olenasha amewahi kupata Tuzo ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ya Mwanafunzi Bora wa Kitivo cha Sheria mwaka 1996/1997.

 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page