Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Profiles Cheo

Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda

Utumishi:
2008 - 2015 (Waziri Mkuu wa Tanzania)

Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1948-08-12
Mahali pa Kuzaliwa: Rukwa Region.

Ndoa: AmeoaMaelezo


Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka Februari 8, 2008 hadi Novemba 2015. Alizaliwa Agosti 12, 1948  mkoani Rukwa. Mh. Pinda alisoma shule ya msingi Kakuni na seminari ya Kaengesa, 1957 – 1964, na baadaye kujiunga na sekondari ya St. Francis, sasa Pugu Sekondari, 1965 – 1968. Alijiunga na Sekondari ya Juu ya Musoma, 1969 – 1970.

Mh. Pinda alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo na kuhitimu, alipangiwa kufanya kazi ya Wakili wa Serikali katika Wizara ya Sheria alikodumu kwa miaka minne kabla ya kuhamishiwa Ikulu kuwa Katibu Myeka Msaidiziwa Rais Julius Nyerere na baadaye Ali Hassan Mwinyi kati ya 1978 na 1995.

Mh. Pinda alihudumu kama Karani wa Baraza la Mawaziri wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa kutoka 1995 hadi 2000. Alijiunga na siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2000 alipopata ubunge wa Jimbo la Mpanda Mashariki, Mkoa wa Rukwa. Aliteuliwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mwaka 2000, na baadaye katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa Januari 4, 2006, Pinda alifanywa waziri kamili  Ofisi ya Waziri Mkuu akishughulikia wizara hiyo hiyo .

Mh. Pinda aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Februari 8, 2008 na kuapishwa rasmi Febrauari 9, 2008 kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa. 

 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page