Sayansi na Teknolojia


Hotuba ya Bajeti Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu

 


Sayansi na teknolojia ni vyombo vyenye nguvu sana katika maendeleo. Katika Tanzania, Sayansi na Teknolojia vimetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya uchumi. Baadhi ya michango hii ni :- 

· Uboreshaji wa tija kwa kubadilisha miundo ya mfumo wa uzalishaji ambayo imeleta ufanisi na ubunifu katika shughuli za kiuchumi.

· Kuongeza mazao ya kuuza nje kwa kuboresha ubora na kupunguza gharama za uzalishaji.

· Kuongeza akiba ya chakula kwa kutoa habari za kitaalamu kwa wazalishaji katika kilimo, na kutoa masoko ya uhakika kwa mazao yao.

· Kusambaza nafasi za kujipatia kipato kwa kutoa taarifa za kitaalam kupatikana kwa wawekezaji wadogo wa mijini na vijijini.

· Kuinua viwango vya ujuzi, wa kiufundi, mwelekeo na tija ya nguvukazi kupitia elimu ya sayansi na teknolojia, na kuisambaza.

Hapo awali, Tanzania ilikuwa haina mpango wala utaratibu wa kuchagua, kujitwalia na kuhamisha teknolojia ambayo ingeingizwa kwenye teknolojia yetu kutokana na utafiti na maendeleo. Lakini, hivi sasa, hatua za makusudi zinafanywa kuhakikisha kuwa uhamishaji teknolojia unaenda kwa kasi, unafaa na ni endelevu, kwa mfano uanzishaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia mwaka 1986 na Kituo cha Maendeleo ya Uhamishaji Teknolojia mwaka 1994, ni kati ya jitihada za kujenga uwezo wa kuratibu, kuchagua, kutwaa, kuendeleza, utafiti, ubadilishanaji habari na huduma za ugani.

Miundombinu ya Sayansi na Teknolojia


Tanzania ina miundombinu kadhaa ya elimu ya sayansi na teknolojia na taasisi za utafiti na maendeleo katika sekta nyingi za kiuchumi.

Baadhi ya vituo vya Elimu ya Sayansi na Teknolojia ni: -

¨ Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 
¨ Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
¨ Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo
¨ Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba na Afya, Muhimbili
¨ Taasisi ya Rasilimali ya Maji ya Rwegalulira
¨ Taasisi za Teknolojia, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam

Baadhi yaVituo vya Utafiti na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia vinavyotoa huduma ni: -

¨ Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini
¨ Taasisi ya Uchunguzi wa Tiba
¨ Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, Serengeti
¨ Shirika la Viwango Tanzania
¨ Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania
¨ Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda.
¨ Taasisi ya Utafiti wa Viuadudu Vya Tropiki

Sera

Sera ya kwanza ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ilianzishwa mwaka 1985 na kuanza kutumika mwaka1995. Mkazo mkubwa wa sera hii ulikuwa kuweka mipango yenye kutoa elimu mpya na kuweka mikakati ya matumizi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini.

Sera ya Sayansi ya Teknolojia kwa hiyo ilikuwa ni chombo cha kuendeleza na kusimamia Sayansi na Teknolojia kwa namna ambayo inaendana na majaliwa ya rasilimali za nchi.


Malengo Makuu ya Sera ya Sayansi na Teknolojia Tanzania ni: -

¨ Kuendeleza sayansi na teknolojia kama nyenzo ya maendeleo ya uchumi, uboreshaji wa maisha ya watu na kulinda uhuru wa nchi.
¨ Kuendeleza kujitegemea kisayansi na kiteknolojia katika utekelezaji wa uchumi kwa kukuza utafiti wa maendeleo
¨ Kuendeleza na kuhamasisha sekta za umma na binafsi za uzalishaji kuendeleza Sayansi na Teknolojia
¨ Kukuza ushiriki wa wanawake katika Sayansi na Teknolojia
¨ Kuanzisha na kuimarisha Taasisi za Taifa za Sayansi na Teknolojia.

Vyama vya Kitaaluma:

Serikali ya Tanzania inaunga mkono uanzishaji na uimarishaji wa vyama kitaaluma, klabu za sayansi, na akademia za sayansi katika taasisi za elimu ili kukuza utamaduni wa sayansi, mwamko wa wananchi na maendeleo kwa jumla ya sayansi na teknolojia. Inatarajiwa kuwa,jumuiya hizi zitachukua jukumu la kutangaza na kueneza sayansi na teknolojia kupitia semina, warsha, mihadhara, filamu na machapisho mbalimbali.

Vyama vya Kitaaluma ni pamoja na: -

¨ Huduma ya Vyuo Vikuu Duniani - hutoa msaada wa masomo kwa watu maskini na wengine waliokosa fursa ya kusoma.

¨ Chama cha Wataalamu wa Eksirei Tazanania - ni chama cha wataalamu wa upigaji picha za eksirei na wasaidizi waliosomea kazi hii.

¨ Chama cha Maarifa ya Nyumbani - hukuza mvuto wa wanachama katika Maarifa ya Nyumbani kama taaluma.

¨ Chama cha Wauguzi Tanzania - huinua kiwango cha elimu ya wauguzi na utendaji.

¨ Chama cha Afya ya Jamii Tanzania - huleta pamoja watu wanaofanya kazi za afya au wenye kupenda taaluma hiyo.

¨ Chama cha Waalimu Wataalamu Tanzania - hukuza taaluma ya ufundishaji na kudumisha maadili na viwango vya juu vya uadilifu na taaluma.

¨ Baraza la Taifa la Utafiti Tanzania - linachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia sayansi na teknolojia.

¨ Chama cha Wasanifu Majengo



Washikadau:

Baadhi yao ni: -

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
S.L.P. 35091
Dar es Salaam

Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Tiba Muhimbili
S.L P 65001
Dar es Salaam

Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo
S.L.P. 35176
Dar es Salaam

Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
S.L.P. 65074
Dar es salaam

Chuo Kikuu Huria Tanzania
S.L.P. 9213
Dar es Salaam

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam
S.L.P. 2958
Darves Salaam

¨ Chuo cha Ufundi Mbeya
S.L.P. 131
Mbeya

Wengine ni: -

¨ Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini
¨ Taasisi ya Utafiti wa Madawa
¨ Utafiti wa Wanyamapori Serengeti
¨ Shirika la Viwango Tanzania
¨ TEMDO
¨ Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania
¨ TIRDO
¨ TISCO
¨ Taasisi ya Utafiti wa Wadudu


Mfumo wa Sera za Teknolojia:

Kamati ya kumshauri Rais juu ya sayansi na teknolojia imeundwa ikiwa ni pamoja na Kamati ya Kiufundi ya Baraza la Mawaziri.

Mfumo wa sheria umewekwa chini ya sheria ya uwekezaji ya mwaka 1990, na ile ya Tume ya Sayansi na Teknolojia No. 7491986 ambayo ilianzisha kituo cha Taifa cha Maendeeleo na Uhamasishaji wa Teknolojia. Kituo hiki kimepewa jukumu la kuweka taratibu na kanuni za kurahisisha upatikanaji, tathmini, uteuzi, uratibu na uendelezaji wa teknolojia.

Ili kufikia lengo la Taifa la kukua kwa uchumi imara, matumizi kamili ya rasilimali na teknolojia, upanuzi wa elimu ya ufundi kwa kukuza vitengo vya utafiti katika shughuli mbalimbali, na sera kamilifu za muda mrefu zenye kuwiana na mipango ya Taifa ya maendeleo, yametekelezwa na serikali ya Tanzania.

Title

.

Title

.

Title

.