SERA YA HABARI NA UTANGAZAJI
(1)
Kila mtu yuko
huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na
kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya
nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2)
Kila raia
anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na
duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya
masuala muhimu kwa jamii.
Aidha,
kutoa na kupokea habari kunatambuliwa duniani kote kuwa ni moja ya haki za
binadamu. Umoja wa Mataifa, na Umoja wa
Afrika zina matamko rasmi ambayo serikali imeridhia kuhusu haki ya kupokea na
kutoa habari. Haki hii,
Dhima
ya Sekta ya Habari na Utangazaji katika jamii ni kutoa habari, kuelimisha na
kuburudisha. Sekta hii inahudumiwa na
vyombo vya habari ambavyo ni redio, magazeti, majarida, televisheni, filamu,
video, intaneti, picha, vipeperushi, katuni na mabango. Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano
yamerahisisha upataji na utoaji habari.
Sekta hii imekua
Asilimia
kubwa ya magazeti na machapisho mengine husomwa zaidi mijini ambako usambazaji
ni rahisi, na kiwango cha kujua kusoma na kuandika ni kikubwa.
Baadhi
ya Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya na Miji zimeanzisha vituo vya
televisheni ambavyo hugharamiwa na halmashauri hizo.
Aidha
yapo magazeti na majarida yatolewayo na Asasi Zisizokuwa za Kiserikali na
mashirika ya dini, ambayo mara nyingi hugharamia vyombo vyao vya habari.
Intaneti
imeanza kuingia kwa nguvu nchini, na miji mingi sasa ina huduma hiyo. Hadi
Desemba, 2002, kulikuwa na makampuni 21 ya huduma za intaneti (
Idara
za serikali, mashirika, na asasi za aina zote zinajitahidi kuwa na tovuti zao,
ili wananchi wapate habari za vyombo hivyo kupitia mtandao huo wa kompyuta.
Tasnia
ya habari ina vyama vya aina nyingi vilivyoundwa na wanahabari wenyewe. Kuna vyama vya kitaaluma, vyama vya
kutetea maslahi na hali bora, kulinda maadili
na uhuru wa vyombo vya habari, vyama vya kuendeleza maslahi ya wanahabari
wanawake na kadhalika. Aidha, zipo klabu
za waandishi wa habari katika mikoa mingi.
Hadi kufikia Desemba, 2002 mikoa
18 ilikuwa na klabu za waandishi wa habari, ambazo, licha ya kuratibu masuala
ya taaluma ya habari katika mikoa, pia zinachangia katika kuhamasisha maendeleo
ya wananchi.
Serikali
ina Idara ya Habari (MAELEZO), ambayo wajibu wake umeainishwa katika Kanuni ya
Kudumu C.16, na Sheria iliyofuta SHIHATA Na. 7 ya Mwaka 2000. Idara hii ina ofisi katika baadhi ya mikoa ya
Tanzania Bara. Aidha, Wizara zote
zimeteua maofisa watakaoshughulikia habari, elimu na mawasiliano. Kuwepo kwa maofisa hao katika wizara na
asasi, mashirika na makampuni mbalimbali huleta uhusiano mzuri kati ya watoaji
na watumiaji wa huduma hizo.
·
Sera ya mwaka
1993 kutoeleza kwa ufasaha nafasi ya Sekta ya Habari na Utangazaji katika
maendeleo ya taifa kwa jumla. Matokeo
yake ni kwamba bado kuna baadhi ya watu wenye mtazamo wa kuona chombo cha
habari kuwa nyenzo ya kufanikisha malengo
·
Baadhi ya
vipengele vya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na Sheria ya Utangazaji ya Mwaka
1993 vina upungufu mkubwa ambao umesababisha malalamiko mengi.
·
Kuna
malalamiko mengi dhidi ya maelekezo kwamba vituo binafsi vya redio na
televisheni vitangaze katika eneo lisilozidi asilimia 25 ya nchi. Serikali ilitoa maelekezo hayo mwaka 1994 kwa
mujibu wa Sheria ya Utangazaji Na.6 ya Mwaka 1993 kwa
lengo la kulinda maslahi ya Taifa kutokana na uchanga wa tasnia ya utangazaji binafsi hapa nchini. Baada ya miaka 10 ya utangazaji binafsi na kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano, serikali imeshauriwa kuangalia upya maelekezo hayo.
·
Hivyo,
madhumuni ya kuwa na Sera Mpya ya Habari na Utangazaji ni kuondoa mapungufu
yaliyojitokeza ili sera hiyo iendane na mazingira mapya ya kisiasa, mabadiliko
ya kiuchumi na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano duniani.
1.0
DIRA NA MALENGO YA SERA YA HABARI NA
UTANGAZAJI
1.1
Dira ya Sera
Dira
ya sera hii ni kuwepo kwa vyombo vingi vya habari, vinavyomilikiwa na umma na
sekta binafsi, na vilivyo imara na anuwai, na vinavyozingatia maadili ya
taaluma na ya jamii, ili viweze kuchangia katika kufanikisha malengo ya Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025.
Aidha, dira ya sera hii mpya inahimiza kuwepo kwa taasisi za mafunzo, utafiti na ushauri wa kitaalam kwa lengo la kuboresha tasnia ya habari na zinazochangia kukuza sekta ya filamu na video, kwa minajili ya kuibua na kukuza vipaji na kulinda historia na utamaduni wa Tanzania.
Sera pia inaelekeza
kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyosambaa nchi nzima.
1.2
Malengo/Madhumuni ya Sera
Madhumuni na Malengo
ya Sera ya Habari na Utangazaji ni
·
Kuweka
mazingira yanayowezesha ukuaji wa Sekta ya Habari na Utangazaji nchini kote;
·
Kuhamasisha
vyombo vya habari kutoa huduma kwa kuzingatia maadili ya taaluma na maadili ya
jamii;
·
Kuhamasisha
wanahabari kuanzisha na kuendeleza chombo cha kusimamia maadili ya taaluma ya
Habari na Utangazaji;
·
Kuweka
utaratibu wa kujenga uwezo endelevu katika sekta.
2.0
MALENGO NA MATAMKO YA SERA
2.1.0 HAKI, UHURU NA WAJIBU WA VYOMBO
VYA HABARI
Hivi sasa upatikanaji wa haki ya kikatiba ya uhuru wa kutoa na kupokea habari unategemea sheria ambazo zinalalamikiwa kuwa zinaondoa haki hiyo, kwa mfano Sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya Mwaka 1970, Sheria ya Magazeti Na. 7 ya Mwaka 1976, Sheria ya Utangazaji Na. 6 ya Mwaka 1993 na sheria nyinginezo zinazohusiana na Sekta ya Habari na Utangazaji. Aidha, vyombo vya habari vya Serikali na binafsi haviwafikii wananchi wote kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Serikali na sheria na kanuni zilizopo. Vilevile, kuna ukosefu wa miundombinu ya mawasiliano na uelewa mdogo wa dhana ya uhuru na wajibu wa vyombo vya habari miongoni mwa wamiliki, watendaji wa vyombo hivyo na wananchi.
2.1.1 Malengo ya Sera
·
Kuondoa
vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa haki ya wananchi ya kupokea na kupata
habari;
·
Kuelimisha
wananchi kuhusu haki
·
Kuhamasisha
uanzishwaji wa vyombo vya habari nchini kote;
·
Kuhamasisha
uwekezaji katika miundombinu ya mawasiliano kote nchini;
·
Kuhamasisha
na kuelimisha wamiliki na watendaji wa vyombo vya habari kuhusu wajibu wa
vyombo vya habari kwa jamii.
2.2
SHERIA ZA VYOMBO VYA HABARI
Kuna malalamiko
kwamba Sheria za magazeti na utangazaji zinampa Waziri mwenye dhamana ya habari
na utangazaji mamlaka ya kuadhibu vyombo vya habari ambavyo vinachapisha au
kutangaza taarifa ambazo, kwa tafsiri yake Waziri, zinatishia maslahi ya umma.
2.2.1 Malengo ya Sera
Kupitia Sheria
zinazolalamikiwa ili:
·
Kuwezesha
wananchi kufaidi kwa ukamilifu haki ya msingi ya kupata na kutoa habari
·
Kulinda
wanahabari wanaotekeleza wajibu wao kwa mujibu wa maadili ya taaluma na ya
jamii;
·
Kulinda haki,
uhuru na wajibu wa vyombo vya habari;
·
Kutoa nafasi
sawa kwa wawekezaji katika sekta ya habari;
·
Kuondoa usiri
usio wa lazima.
2.2.2
Maelekezo ya Sera
·
Serikali
itahakikisha sheria za vyombo vya habari zinazolalamikiwa zinadurusiwa na
kurekebishwa;
·
Serikali
itahakikisha kuwa sheria za vyombo vya habari zinazingatia haki ya kusuluhishwa
kupitia mkondo wa Mahakama;
·
Serikali
itasimamia kutungwa kwa sheria moja inayotawala vyombo vya habari.
2.3
UMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI
Hivi sasa mmiliki mmoja anaruhusiwa kuwa na zaidi ya chombo kimoja cha habari. Aidha, baadhi ya vyombo vya habari vimeanzishwa bila watendaji wenye taaluma. Wamiliki wengine wa vyombo vya habari hawatoi mafunzo kazini kwa watumishi wao. Vilevile, baadhi ya vituo vya redio na televisheni vinatumiwa na wawekezaji na mashirika ya habari ya nje kueneza sera na utamaduni wa mataifa ya nchi za nje na hivyo kuathiri mila na utamaduni wetu. Baadhi ya wawekezaji hao wa nje pia wanadhibiti maudhui ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini, na hivyo kuathiri mtazamo wa kizalendo wa wananchi.
2.3.1
Malengo ya Sera
·
Kuendelea
kuruhusu mmiliki mmoja kuwa na zaidi ya chombo kimoja cha habari;
·
Kuvifanya
vyombo vya habari vizingatie wajibu wa kutoa huduma kwa manufaa ya umma;
·
Kuhakikisha
mmiliki wa chombo cha habari ana watendaji wenye taaluma;
·
Kuwahamasisha
wamiliki wa vyombo vya habari kuwaendeleza watumishi wao kitaaluma;
·
Kuhakikisha
kwamba uendeshaji wa vyombo vya habari unakuwa mikononi mwa Watanzania, na
wageni wanaajiriwa tu
2.3.2
Maelekezo ya Sera
·
Serikali
iendelee kuwaruhusu wamiliki kuwa na zaidi ya chombo kimoja cha habari;
·
Raia wa nchi
za nje wanaweza kuwekeza katika chombo cha habari kwa ubia na raia, ili mradi
hisa za Mtanzania zisiwe chini ya asilimia 51 kumwezesha kuongoza chombo hicho
wakati wote;
·
Uendeshaji wa
vyombo vya habari utakuwa mikononi mwa Watanzania;
·
Wageni
wataajiriwa tu
·
Serikali
iwahamasishe wawekezaji kuanzisha vyombo vya habari katika maeneo ambayo
hayavutii kibiashara;
·
Chombo cha
habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji, bali kitatumiwa
kwa maslahi ya umma;
·
Chombo cha
habari kiongozwe na maadili ya taaluma na ya jamii husika;
·
Chombo cha
habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia
au ulemavu au kuchochea uhasama;
·
Lugha
zitakazotumiwa na vyombo vya habari hapa nchini ni Kiswahili na Kiingereza.
2.4
SERIKALI NA HABARI
Baadhi
ya wananchi hivi sasa hawapati huduma ya habari kupitia vyombo vya habari vya
Serikali kwa kuwa baadhi ya maeneo ya nchi hayana miundombinu ya
mawasiliano. Aidha, dhana ya uwazi na
ukweli haitekelezwi ipasavyo kutokana na sheria, kanuni na taratibu za usiri
Serikalini. Vilevile kuna migongano ya
taarifa zitolewazo na taasisi mbalimbali za Serikali. Kutoshirikishwa kwa Idara ya Habari kama
Msemaji Mkuu wa Serikali katika vikao vinavyotoa maamuzi mbalimbali na ukosefu wa watendaji wenye taaluma
ya habari katika Wizara, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa hufanya Serikali
kushindwa kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu yake kwa ukamilifu kwa
wananchi kupitia vyombo vya habari.
2.4.1 Malengo ya Sera
·
Kuimarisha
huduma za vyombo vya habari vya Serikali nchini kote, na hasa katika maeneo
yasiyopendelewa na wawekezaji binafsi;
·
Kuondoa
vikwazo vya upatikanaji wa habari Serikalini na taasisi zake;
·
Kuendeleza
Idara ya Habari
·
Kuimarisha
vitengo vya habari vya wizara, idara na taasisi za Serikali, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa;
·
Kuweka
utaratibu wa Msemaji wa Serikali katika ngazi za wizara, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali;
·
Kuimarisha
taasisi za Serikali za kutoa mafunzo ya taaluma ya habari.
2.4.2
Maelekezo ya Sera
·
Serikali
iendelee kumiliki vyombo vya habari na kuwekeza katika huduma za habari kote
nchini;
·
Serikali
iendelee kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha vyombo vya habari kote nchini;
·
Serikali
iondoe vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa habari za manufaa kwa wananchi;
·
Serikali
iendelee kuwa na wasemaji wake katika ngazi za taifa, wizara, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa na taasisi za Serikali;
·
Serikali
iimarishe Idara ya Habari ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
2.5 MAGAZETI
NA MAJARIDA
Hivi leo, kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya taaluma ya
uandishi wa habari na ya jamii na uanzishwaji holela wa vijarida. Pia asilimia kubwa ya nchi haina huduma ya
magazeti na gharama za huduma za magazeti hivi sasa ni kubwa. Aidha, baadhi ya magazeti na majarida yanachapisha
taarifa na picha zinazochochea uvunjaji wa maadili
2.5.1 Malengo ya Sera
·
Kuhakikisha
magazeti na majarida yanazingatia maadili ya taaluma na maadili ya jamii na
kuhakikisha kwamba magazeti na majarida yote yanasajiliwa kwa mujibu wa sheria;
·
Kutafuta njia
za kupunguza bei za magazeti;
·
Kuhimiza
uzingatiaji wa maadili ya jamii na ya taaluma ya uandishi wa habari.
2.5.2
Maelekezo ya Sera
·
Magazeti na
majarida yataendelea kusajiliwa na Serikali kwa mujibu wa sheria;
·
Serikali
itaendelea kuzihamasisha taasisi na asasi mbalimbali kuanzisha magazeti na
majarida katika maeneo
·
Serikali
ihamasishe wamiliki wa kampuni za uchapishaji kushirikiana katika kutafuta njia
za kupunguza gharama za uchapishaji;
·
Majarida ya
burudani na starehe yatasajiliwa kwa mujibu wa sheria, na yatachapishwa na
kusambazwa kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania na Kanuni zitakazowekwa.
2.6 MASHIRIKA
YA HABARI
Idara
ya Habari ambayo ni moja ya mashirika ya habari, haina rasilimali za kuiwezesha
kutekeleza kikamilifu majukumu ya kihabari yaliyoachwa na Shirika la Habari
2.6.1
Malengo ya Sera
·
Kuhamasisha
sekta binafsi kuwekeza kwenye mashirika ya habari;
·
Kuwezesha
Idara ya Habari kuwa na nyenzo na watalaam wa kutosha kuweza kutekeleza
majukumu yake;
·
Kuhamasisha
uwekezaji kwenye miundombinu ya mawasiliano ya habari.
2.6.2
Maelekezo ya Sera
·
Serikali
iimarishe Idara ya Habari ili itekeleze majukumu yake kwa kuipatia wataalam,
vitendea kazi, na nyenzo nyingine;
·
Sekta binafsi
ihamasishwe kuwekeza kwenye mashirika ya habari;
·
Serikali
ihamasishe na kushirikisha sekta binafsi kuwekeza kwenye miundombinu ya habari
na mawasiliano.
2.7
REDIO, TELEVISHENI NA INTANETI
·
Hivi sasa
intaneti haitawaliwi na sheria yoyote nchini, baadhi ya vipindi vya redio na
televisheni havizingatii maadili ya Kitanzania, maeneo mengi ya vijijini hayana
huduma ya televisheni na vituo vingi vya utangazaji vina vipindi vichache
vyenye maudhui ya Kitanzania kwa kuwa watumishi wengi wa vituo hivyo hawana
taaluma ya kutosha. Vilevile hakuna
utaratibu maalum kwa vituo binafsi vya redio na televisheni kujiunga na vituo
vya Serikali katika kutangaza matukio maalum ya kitaifa.
2.7.2
Malengo ya Sera
·
Kuweka huduma
za intaneti chini ya sheria na taratibu zinazotawala huduma za redio na
televisheni;
·
Kuhakikisha
kuwa maudhui ya vipindi vya redio na televisheni yanazingatia maadili ya
taaluma na ya jamii;
·
Kuhamasisha
kuanzishwa kwa huduma ya televisheni maeneo ya vijijini;
·
Kuhamasisha
vituo vya redio na televisheni kuajiri watumishi wenye taaluma ya habari na
utangazaji;
·
Kuweka
utaratibu wa vituo binafsi ya redio na televisheni kujiunga na redio na
Televisheni ya Taifa kutangaza matukio maalum ya kitaifa.
2.7.3
Maelekezo ya Sera
·
Redio,
televisheni na intaneti ziendelee kusajiliwa kwa mujibu wa sheria;
·
Vituo vya
redio na televisheni na intaneti vitatakiwa kuzingatia maadili ya taaluma na ya
jamii na utamaduni wa
·
Redio na
televisheni za binafsi zitangaze katika eneo lolote la nchi kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za utangazaji zitakazowekwa na mamlaka za usimamizi wa
utangazaji;
·
Maudhui ya
vipindi vya redio na televisheni yaimarishe amani, umoja, mshikamano na usalama
wa taifa;
·
Vituo vya
redio na televisheni vizingatie athari za matumizi ya vipindi vya nje kwa
utamaduni na maadili ya Taifa;
·
Lugha za
kurushia matangazo ya redio na televisheni nchini ni Kiswahili na Kiingereza;
·
Redio na
televisheni binafsi zishiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa na katika
kampeni za taifa na maafa;
·
Vituo vya
intaneti vijitahidi kuwaepusha watoto na athari mbaya za intaneti;
·
Utoaji wa
masafa ya kutangazia uzingatie vigezo vitakavyowekwa na mamlaka ya usimamizi wa
utangazaji;
·
Serikali
iweke utaratibu wa vituo binafsi vya redio na televisheni kujiunga na redio na
Televisheni ya Taifa kutangaza matukio maalum ya Kitaifa.
2.8 FILAMU,
VIELELEZO NA VIDEO
Baadhi ya filamu, video na vielelezo vilivyopo vinachochea vitendo vya ngono na baadhi ya filamu, video na vielelezo vinachochea ubaguzi kwa misingi yakabila, jinsia na dini na pia baadhi ya filamu, video na vielelezo vinachochea fujo, utumiaji wa madawa ya kulevya na unyanyasaji wa jinsia.
2.8.1
Malengo ya Sera
·
Kuhakikisha
kuwa uonyeshaji wa filamu, vielelezo na video unazingatia maadili ya taaluma ya
habari na ya jamii;
·
Kuhamasisha
utengenezaji wa filamu, video na vielelezo vyenye maudhui ya Kitanzania;
·
Kukuza vipaji
vya wananchi katika fani za filamu, video na vielelezo;
·
Kuhamasisha
uwekezaji katika tasnia ya filamu, video na vielelezo.
2.8.2
Maelekezo ya Sera
·
Wamiliki na
waendeshaji wa shughuli za filamu, video na vielelezo wasieneze ubaguzi wowote,
uchochezi wa kisiasa na kidini au udhalilishaji wa kikundi chochote cha jamii
ya Watanzania. Aidha, wahakikishe kuwa
silka, maadili, utamaduni na utu wa Mtanzania vinadumishwa na kuheshimiwa;
·
Asasi zinazotengeneza
filamu, video na vielelezo, ziendeleze vipaji vya Watanzania katika fani
mbalimbali na kudumisha utamaduni wao;
·
Mamlaka
zinazohusika, zisimamie kwa ukamilifu utekelezaji wa sheria zinazotawala
maonyesho filamu, video na vielelezo;
·
Sanaa na taaluma
ya filamu, video na vielelezo iendelezwe.
2.9 KUJENGA
UWEZO WA SEKTA
Wanahabari wengi hawana mafunzo ya taaluma kwa kuwa kuna
vyuo vikuu vichache vinavyotoa taaluma ya habari na ambavyo havikidhi mahitaji
ya taifa. Aidha, vyuo vingi vya watu binafsi
havina makazi ya kudumu, havina mitaala, havina vifaa vya kufundishia vya
kutosha na havina walimu wenye elimu ya juu na uzoefu wa kutosha. Hivyo, mafunzo yatolewayo na baadhi ya
taasisi za habari ni ya ngazi ya chini kiasi kwamba hayafikii kiwango cha
taaluma kinachotakiwa. Pia, kutokana na
utata wa sheria uliopo vyuo vya binafsi vya kufundisha wanahabari vimeanzishwa
2.9.1
Malengo ya Sera
·
Kuwezesha
sekta ya habari kuwa na taasisi imara za mafunzo na utafiti;
·
Kuinua
viwango vya taaluma vya wanahabari;
·
Kuwezesha
vyombo vya habari kuwa na watendaji wengi na bora ili kukidhi mahitaji ya soko;
·
Kuwezesha
kupatikana kwa watendaji wenye ujuzi na mbinu za kumudu ushindani kutoka vyombo
vya habari vya nje ya nchi;
·
Kudumisha
uzingatiaji wa maadili ya taaluma na ya jamii.
2.9.2
Maelekezo ya Sera
·
Mafunzo ya
wanahabari yalenge katika ngazi ya elimu ya juu;
·
Vyuo Vikuu
vya Serikali vianzishe mafunzo ya taaluma yatakayotosheleza fani zote za sekta
ya habari na utangazaji;
·
Taasisi za
mafunzo ya taaluma ya habari na utangazaji zitilie mkazo elimu ya utafiti
itakayosaidia kutatua matatizo ya maendeleo ya sekta ya habari;
·
Mafunzo ya
taaluma ya habari yatolewe na vyuo na taasisi zilizoidhinishwa na vyombo vya
usimamizi wa Elimu ya Ufundi na Elimu ya Juu;
·
Mafunzo
kazini yawe ni haki ya mwanahabari.
Mafunzo hayo yalenge kuinua kiwango cha elimu na ujuzi, kuongeza upeo wa
masuala ya kijamii na kupata elimu ya teknolojia mpya.
3.0
MGAWANYO WA MAJUKUMU
Katika utekelezaji
wa Sera ya Habari na Utangazaji, Serikali na asasi mbalimbali zitatekeleza
majukumu yafuatayo:
3.1
Serikali
·
Kulinda haki
ya msingi ya mwananchi ya kupata habari iliyotajwa katika Ibara ya 18 ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa
·
Kuweka
mazingira yatakayowezesha kuimarika kwa Sekta ya Habari na Utangazaji;
·
Kuratibu,
kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Sera.
3.2
Baraza la Habari
·
Litaimarisha,
litadumisha na kuendeleza maadili na viwango vya utendaji katika vyombo vya
habari na utangazaji;
·
Litashirikiana
na wadau katika kukuza haki, uhuru na wajibu wa vyombo vya habari;
·
Litaleta
uhusiano mwema baina ya wananchi na vyombo vya habari, na baina ya vyombo
vyenyewe.
3.3 Vyama vya Wanahabari
·
Vitasaidia
wanachama kupata taaluma katika fani zao;
·
Vitainua
kiwango cha ufanisi na utendaji katika Sekta ya Habari;
·
Vitahamasisha
maelewano baina ya wanahabari na vyanzo vya habari;
·
Vitaelimisha
jamii kuhusu haki
·
Vitatetea
maslahi ya wanachama wao.
3.4
Vyombo vya habari
·
Vitatoa
huduma za habari, elimu na burudani kwa kuzingatia maadili na utamaduni wa
Mtanzania;
·
Vitachangia
kuinusuru jamii kutokana na majanga
·
Vitashiriki
katika kampeni za kuendeleza jamii katika nyanja mbalimbali,
3.5
Taasisi za Mafunzo
·
Zitajenga
uwezo wa wanahabari kwa kutoa mafunzo ya fani za habari na utangazaji kulingana
na mahitaji ya Sekta ya Habari na Utangazaji;
·
Zitafanya
utafiti wa masuala mbalimbali kwa madhumuni ya kuendeleza Sekta ya Habari na
Utangazaji.
3.6
Wamiliki wa vyombo
·
Watahakikisha
vipindi havikiuki maadili;
·
Wataandaa
programu za mafunzo.
3.7
Vyombo vya Usimamizi
Usimamizi wa Sekta ya Habari na
Utangazaji unafanywa na Serikali kupitia Mamlaka mbalimbali za usimamizi wa
vyombo vya habari na utangazaji.
·
Mamlaka hizo
za Serikali zitasimamia utekelezaji wa Sheria ya vyombo vya habari na
utangazaji na kuratibu vyombo hivyo ili kuvisaidia viimarike na viendelee
kuwahudumia wananchi. Aidha serikali
itaendelea kusimamia siyo tu uhuru bali pia uwajibikaji wa vyombo hivyo vya
habari kwa jamii kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na maadili ya jamii na
ya taaluma ya habari;
·
Baraza la
Habari litaendelea kulinda haki za watumiaji na watoaji wa huduma ya habari; na
kusuluhisha malalamiko yanayotolewa dhidi ya vyombo vya habari na malalamiko ya
wanahabari dhidi ya vyanzo vya habari, taasisi na wanajamii wengine. Aidha, litatoa elimu ya umma kuhusu
umuhimu,haki na wajibu wa vyombo vya habari, litaendelea kuhimiza vyombo vya
habari kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maadili ya jamii na ya taaluma ya
habari, na litaipa Serikali ushauri wa kitaalam kuhusu namna ya kuboresha
mazingira ya sekta ya habari.
4.0
URATIBU NA UFUATILIAJI
4.1
Uratibu
Idara ya Habari ndiyo mratibu wa masuala yote yanayohusu habari na utangazaji hapa nchini. Ni jukumu la Idara ya Habari kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa Sera hii utakaokuwa unafanywa na vyombo mbalimbali.
4.2
Vigezo vya tathmini
Kufanikiwa kwa Sera
Mpya ya Habari na Utangazaji kutapimwa kutokana na vigezo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na:
·
Uelewa wa wananchi
wa haki ya kupata na kutoa habari ilivyo katika Katiba au
·
Uongezekaji
wa wasomaji wa magazeti, wasikilizaji wa redio, watazamaji wa televisheni na
video na watumiaji wa intaneti, hasa vijijini;
·
Uongezekaji
wa Watanzania wanaomiliki magazeti, vituo vya redio, televisheni, intaneti na
mashirika ya habari;
·
Kudurusiwa
kwa sheria zinazoathiri utendaji wa Sekta ya Habari na Utangazaji;
·
Kutungwa kwa
sheria moja ya vyombo vya habari na utangazaji;
·
Kuongezeka
kwa maudhui ya Kitanzania katika vyombo vya habari na utangazaji;
·
Kupungua au
kutoweka kwa malalamiko kuhusu uvunjaji wa maadili ya taaluma ya habari na ya
jamii;
·
Kuongezeka
kwa wahitimu wa fani za habari na utangazaji na mawasiliano katika ngazi
mbalimbali;
·
Kuongezeka
kwa wanahabari wenye mafunzo ya taaluma zingine
·
Kuongezeka
kwa vyuo vinavyofundisha taaluma ya habari na utangazaji;
·
Matangazo ya
Redio