Takwimu

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002

Inflation rate for September 2002 has remained the same as was for August 2002. According to the National Consumer Price Index  (NCPI), Inflation rate for September 2002, is 4.4 percent in relation to the figures for September the previous year. The September inflation rate has remained stagnant when compared with August 2002 inflation figure, which was 4.4 percent, as measured on a year-to-year basis. However, as measured on a month-to-month basis, that is between August 2002 and September 2002 inflation went down by 0.6 percent. »»more»»  

National Consumer Price Index September, 2002

¨      Ofisi ya Taifa ya Takwimu

¨      Mfumo wa Kusambaza Data

¨      Chunguzi za Demografia na Afya Tanzania

¨      Sensa ya Taifa ya mwaka 2002

¨      Kituo cha Takwimu za Uchumi na Jamii Tanzania

¨      Mtandao wa Habari za Idadi ya Watu Tanzania

¨      Taasisi za Takwimu Tanzania 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu 

Ofisi ya taifa ya takwimu, kama wakala wa Serikali iliundwa kutokana na ofisi ya zamani ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kutoa huduma kwa ufanisi, ili fedha itolewayo iwe na thamani zaidi kwa manuaa ya Serikali na wananchi kwa jumla.  Ofisi ya Taifa ya Takwimu inafanya kazi zake kibiashara, ikitumia usimamizi wa fedha wa kibiashara, na mbinu za kupanga kibiashara, na inamwelekea zaidi mteja. 

Dira

Dira ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kama wanavyoiona watumishi, ni kuwa chanzo chenye mamlaka na cha kuaminika cha habari za takwimu ihusuyo hali ya jamii na uchumi nchini, taasisi yenye uwezo wa kutoa taarifa inavyotakiwa, mahali pa rejea kwa methodolojia ya takwimu na viwango, na kituo cha kuratibu shughuli za takwimu kwa lengo la kutoa takwimu dhabiti. 

Mwelekeo.

Mwelekeo ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ni kuwezesha upangaji mipango na uchukuaji maamuzi ndani ya Serikali na jumuiya ya kibiashara, kuchochea utafiti na kuarifu umma kupitia takwimu za kuaminika na za wakati, na kutoa huduma bora ya takwimu kwa jumla.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ni wakala pekee mwenye mamlaka ya kutoa takwimu kwa Serikali, jumuiya ya kibiashara na wananchi kwa jumla.  Ofisi ya Taifa ya Takwimu inajitahidi kutekeleza wajibu huu kwa niaba ya Serikalai kwa uadilifu na ufanisi kwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima. Ina uwezo wa teknolojia wa kuweza kutoa huduma ya takwimu kwa Taifa.  Ofisi ya Taifa ya Takwimu iko tayari kukabiliana na changamoto yeyote katika utoaji wa huduma hii kwa kupunguza gharama za uendeshaji, na kugharamia shughuli zake kwa kuweka bei za kuvutia za bidhaa na huduma zitolewazo.  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imedhamiria kutoa huduma za takwimu nchini. 

Anwani 

Ofisi za Takwimu ziko Jengo la Casino Mtaa wa Kivukoni Front.

S.L.P. 796

DAR ES SALAAM.

Simu:    255-22-2122722/3/4/5/,. 2137834, 2111634

Fax:            2112352

Baruapepe: nbs.dg@raha.com

Website: www.nbs.com.tz

Title

.

Title

.

Title

.