|
Nchi
ya Tanzania iko katika pwani ya Mashariki ya Bara la afrika kati
ya longitudo 29 na 41 Mashariki, na Kati ya latitudo l na l2
kusini. Ncha ya
kaskazini kabisa ya nchi ni mji wa Bukoba, usawa wa latitudo l
Kusini; na ncha ya Kusini kabisa ni mji wa Mtalika, usawa wa
latitudo 12 kusini. Ncha
ya Magharibi kabisa ni mji wa kigoma usawa wa longitudo 29
mashariki ya msistari wa Greenwich, na ncha ya Mashariki kabisa ni
mji wa Mtwara ulioko usawa wa Longitudo 41.
Kwa
upande wa kaskazini, Tanzania imepakana na nchi za Kaenya na
Uganda ambapo upande wa magharibi imepatana na nchi za Burundi na
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Kwa upande wa kusini, Tanzania imepakana nchi za Zambia,
Malawi na Msumbiji ambapo upande wa mashariki imepakana na Bahari
ya Hindi.
·
Mazingira
ya Nchi:
Tanzania
ndiyo nchi kubw akupita nchi zote za Afrika mashariki (Kenya,
Uganda na tanzania). Tanzania ina maumbile matatu ya kipekee ambayo ni Visiwa vya
Zanzibar na Pemba na Ukanda wa pwani kwa upande wa mashariki, na
muinuko wenye umbile la bakuli katikakakati, pamoja na nyanda za
juu. Bonde la ufa
(The Greaf Rift Valley) ambalo LINAANZIA Kaskazini-Mashariki ya
Bara la Afrika na kupitia katikati ya Tanzania ndiyo alama
nyingine kubw inayoongeza mandhari ya nchi.
Bonde hilo la ufa limekwenda hadi kufikia kusini katika
Ziwa Nyasa na kujigawa pande mbili, moja ikiendelea Kusini zaidi
ya Ziwa Nyasa hadi Mozambique, na pande nyingine ikielekea
Kaskazini-Magharibi pembezoni mwa Burundi, Rwanda, Tanzania na
sehemu ya Magharibi ya nchi ya Uganda.
Ndani
ya Bonde Kuu hili la ufa, kuna msururu wa maziwa kama vile Ziwa
Rukwa, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, Ziwa Kitangiri, Ziwa Eyasi na
Ziwa Manyara. Sehemu
za miinuko ni pamoja na Kipengere, Udzungwa, Matogoro, Livingstone
na Ufipa ambazo kwa pamoja zinafanya Nyanda za Juu za Kusini.
Safu ya milima ya Usambara, Pare, Meru, Kilimanjaro, Shimo
la Volkeno la Ngorongoro na Oldonyo Lengai vyote hivi ndivyo
vinavyoitwa Nyanda za Juu za Kaskazini.
Kutoka shemu hizi za miinuko pamoja na bonde la Kati ndiko
kunakopita mitiririko ya maji ambayo hatimaye huishia katika
bahari za Hindi, Atlantic na Mediterranean pamoja na maziwa na
mabwawa yaliyomo nchini.
Milima
ya Tanzania:
-
Mlima Kilimanjaro wenye urefu juu ya usawa wa bahari wa
mita 5,895
-
Mlima Meru, mita 4566
-
Mlima Rungwe, mita 2,960
-
Milima ya Uluguru, mita 2,648
-
Milima ya Rubeho, mita 2,576
-
Milima ya Livingstone, mita 2,521
-
Mlima Mbizi, mita 2,418
-
Mlima Mahari, mita 2,373
-
Milima ya Usambara, mita 2,300
Hali
ya Hewa:
Nchi
ya Tanzania ni ya hali ya joto (tropical type of climate).
Katika nyanda za juu hali ya joto inaanzia nyuzi joto 10
hadi 20 wakati wa baridi na joto.
Sehemu nyingine zilizobakia nchini joto lake mara nyingi
halipungui chini ya nyuzi joto 20.
Kipindi chenye joto kali ni kati ya mwezi Novemba na
Februari (Nyuzi joto 25-31) na kipindi cha baridi kali ni kuanzia
mwezi Mei hadi Agosti (Nyuzi joto 15-20).
Kuna misimu miwili ya mvua katika Tanzania. Msimu wa kwanza ambao una mvua fupi peke yake unaanzia mwezi
Desemba hadi Aprili; na msimu mwingine wenye mvua fupi na ndefu ni
kati ya Mwezi Oktoba na desemba, halafu kati ya Machi na Mei.
Katika
msimu wa pili, mvua za mwezi Machi hadi Mei zinaitwa mvua za
masika (mvua ndefu) wakati zile za miezi ya Oktoba hadi desemba
zinajulikana kwa jina la mvua za vuli, au mvua fupi.
Maelezo
kuhusu Tanzania:
·
Eneo:
Tanzania
nzima ina eneo la nchi kavu la kilomita za mraba 945,000 ambazo
kati ya hizo, Kilomita za mraba 881,000 ni eneo la Tanznaia Bara
peke yake, na kilomita za mraba 2,000 ni eneo la visiwa vya
Zanzibar na Pemba. Eneo
lililofunikw ana maji kwa nchi nzima ni Kilomita za mraba 62,000
na eneo la mwiktu na pori ni kilomita za mraba 3,350.
·
Mfumo
wa Siasa: Dekokrasia ya vyama vingi
·
Utawala: Kuna mikoa ya utawala 25 (Bara 20 na Zanzibar 5), wilaya za
utawala 123 (Zanzibar 10 na Bara 113).
·
Idadi
ya Watu: Tanzania nzima inakadiriw akuwa na jumla ya watu milioni 32
(makisio ya mwaka 2001). Kati
ya idadi hiyo yote, asilimia 51 ni wanawake na asilimia 46 ni
watoto walio na umri chini ya miaka 15.
·
Umasikini: Takriban asilimia 50 ya idadi ya watu wote nchini wanaishi
maisha ya ufukara.
·
Pato
la Taifa kwa mtu mmoja: Dola za Kimarekani 246 (mwaka 2001).
·
Pato
la Ndani ya nchi kwa mtu mmoja:
Dola za Kimarekani 251 (mwaka 2001).
Maliasili
·
Madini
– dhahabu, almasi, tanzanite, mawe mengine ya thamani, gesi ya
asili, chuma, mkaa wa mawe, maji ya chemchem, nta ya kung’ara,
magadi na chumvi.
·
Wanyama
na Utalii: Mbuga 12
za wanyamak, Eneo la Hifadhi la Ngorongoro, Hifadhi za wanyama 13,
Hifadhi maalum za wanyama 38 na sehemu za hifadhi za utamaduni
120.
·
Uvuvi:
Hufanyika
kwenye maziwa makuu matatu ambayo ni Victoria, Tanganyika na Nyasa
pamoja na mito na pwani ya Bahari ya Hindi. Pato la samaki
linaloweza kupatikana kwa mwkaa mzima linakadiriw akuwa tani za
metriki 730,000 kwa mwaka, ingawa kwa hivi sasa ni tani 350,000 tu
kwa mwaka.
Mji
Mkuu:
Dodoma
ndiyo mji mkuu na Makao makuu ya Serikali ya Tanzania.
Mji huu, wenye idadi ya watu wapatao 300,000 (Makisio ya
mwaka 1998), uko umbali wa kilomita 309 kutoka dar es Salaam
kuelekea mashariki. Dar
es Salaam ndiyo mji mkuu wa kibiashara. Miji mingine mikubw ani Arusha, Moshi, Tanga na Mwanza kwa
upande wa Kaskazini ya nchi, Moarogoro upande wa Mashariki; Mbeya
na Iringa upande wa Magharibi.
Tabora na Shinyanga pia ni miji maarufu kwa shughuli za
kiuchumi nchini Tanzania. Dar
es Salaam na Mwanza ndiyo pekee yenye hadhi ya jiji.
Sikukuu
za Kitaifa (2002)
1
Januari
-
Mwaka Mpya
12
Januari
-
Mapinduzi Zanzibar
11
Machi
-
Idd - Eli - Hadji (yategemea kuandama kwa mwezi)
29
Machi
-
Ijumaa Kuu
1
Aprili
-
Jumatatu ya Pasaka
26
Aprili
-
Muungano wa Tanzania
1
Mei
-
Siku ya Wafanyakazi Duniani
27
Juni -
Maulid (inategemea kuandama kwa mwezi)
7
Julai
-
Sabasaba
8
Agosti -
Siku ya Wakulima
9
Desemba -
Uhuru na Jamhuri
5
na Desemba
- Idd - El - Fitri
(inategemea kuandama kwa
mwezi)
25
Desemba
- Kuzaliwa Kristo
26
Desemba
- Siku ya Kupeana Zawadi
Alama
za Taifa
·
Bendera
ya Taifa:
Uwiano
wa urefu na upana:-
Tatu kwa mbili, mfano ft.3xft.2, ft.6xft.4, ft. 12xft.8.
Ina
rangi za kijani, dhahabu, nyuekusi na bluu, ambapo rangi nyeusi
imepit katikati ya bendera kuanzia pembe ya chini kwenye mlingoti
na kuishia pembe ya juu kulia.
Rngi hii huigawa bendera katika sehemu mbili zenye umbo la
pembe tatu. Rangi nyeusi imetenganishwa na pembe tatu ya juu yenye
rangi ya kijani na pembe tatu ya chini yenye rangi ya bluu kwa
mistari miwili midogo yenye rangi ya dhahabu.
Viwango
vya rngi na maana zake:-
Nyeusi -
Kiwango Na. 9-103
- maana yake ni WATU .
Kijani -
Kiwango Na. 0-010
- maana yake ni ARDHI
Bluu -
Kiwango Na. 0-012
- maana yake ni BAHARI na MAZIWA
Dhahabu
-
Kiwango Na. 0.002
- maana yake ni madini
Uwiano
wa rangi:
Rangi
nyeusi kwa bendera ya Ft. 6xft.4 ni 13/18 kwenda juu n13 upana.
Mistari ya dhahabu ni 1/16 kwenda juu na inchi 3 upana kila
mmoja.
·
Wimbo
wa Taifa
(1)
Mungu ibariki Afrika
Wabariki
viongozi wake
Hekima,
umoja na amani
Hizi
ni ngao zetu
Afrika
na watu wake.
KIBWAGIZO
Ibariki,
Afrika
Ibariki,
Afrika
Tubariki,
watoto wa Afrika.
(2)
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha
uhuru na umoja
wake
kwa waume na watoto
Mungu,
ibariki
Tanzania,
na watu wake.
KIBWAGIZO
Ibariki,
Tanzania
Ibariki,
Tanzania
Tubariki,
Watoto wa Tanzania
|