|
Sekta
ya usafirishaji ina mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na
uchumi Tanzania. Sekta
imeendelea kukua kutokana na juhudi za uwekezaji wa Serikali
pamoja na sekta binafsi katika kukarabati barabara, kukuza
mawasiliano ya simu, kufanya bandari kuwa za kisasa na uboreshaji
wa huduma za usafiri majini, reli na anga.
Usafiri
wa reli.
Mifumo
miwili ya reli inatumika Tanzania. Shirika la Reli Tanzania lina njia mbili: njia ya kati
inayoanzia Dare es Salaam hadi Tabora na kugawanyika kwenda Kigoma
kwa upande wa magharibi kwenye Ziwa Tanganyika, na hivyo kutoa
huduma ya usafirishaji mizigo kwa eneo hilo kwa nchi za Burundi,
Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tawi la pili ni lile la kwenda Mwanza kwenye bandari ya
Ziwa Viktoria, ikitoa pia huduma ya usafirishaji mizigo kwa eneo
la kaskazini na kaskazini-magharibi, ikiwemo Uganda. Njia ya pili ni ile ya kutoka Ruvu kuelekea kaskazini hadi
Korogwe, na kugawanyika kwenda Tanga kwenye bahari ya Hindi na
kaskazini –magharibi hadi Moshi kuunganisha na mfumo wa reli ya
Kenya.
Mfumo
mwingine wa reli ni, reli ya Mamkala ya Reli Tanzania na Zambia-
TAZARA. Hii ni reli
ya pamoja ya nchi za Tanzania na Zambia.
TAZARA inaunganisha bandari ya Dar es Salaam na Zambia
ikisafirisha mizigo ya nchi za Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo na Zambia.
Shirika la Reli Tanzania na Mamlaka ya Reli ya
Tanzania-Zambia yamepangwa kubinafsishwa.
Usafirishaji
Majini
Mamlaka
ya Bandari Tanzania inasimamia bandari za Dar es Salaam, Tanga
Mtwara na Bandari ndogo za Kilwa na Lindi kwenye Bahari ya Hindi.
Dar es Salaam ndiyo bandari kubwa yenye uwezo wa
kusafirisha mizigo mingi.
Kuna
usafirishaji wa maziwa unaoendeshwa na Idara ya Majini ya Shirika
la Reli Tanzania. Kuna
huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria
(kuunganisha Tanzania, Kenya, Uganda), Ziwa Tanganyika
(kuunganisha Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na
Zambia), na kwenye ziwa Nyasa (kuunganisha Tanzania, Malawi,
Msumbiji).
Usafiri
wa Anga
Tanzania
ina viwanja vya ndege vya kimataifa vitatu:
Dar es salaam, Kilimanjaro na Zanzibar.
Zaidi ya hivyo kuna viwanja vingine vya ndege vilivyoenea
nchini nzima. Shirika
la Ndege la Taifa – ATC ni msafirishaji mkuu ndani ya nchi
likiunganisha miji yote mikubwa nchini.
Kampuni binafsi nazo zimeanza kutoa huduma ya kusafirisha
abiria, na pia kuna kampuni za ndege za kukodi.
ATC ina huduma nchi za jirani na Mashariki ya Kati. Pia
kuna ndege za mashirika ya kimataifa zenye kusafiri kati ya
Tanzania na Ulaya, India, Mashariki ya Kati na Kusini mwa Afrika.
Usafiri
wa Barabara
Jiolojia
ya Tanzania, ukubwa wake, uanuwai na mtawanyiko unaipa nafasi
kubwa barabara katika kuunganisha uchumi wa Taifa.
Na hasa barabara huhudumia vijijini (wanakoishi Watanzania
wengi) kwa manufaa zaidi kuliko aina nyingine za usafiri.
Mfumo
wa taifa wa barabara (chini ya Wizara ya Ujenzi) unakabiliana na
ukosefu wa fedha za kukarabati na kuendeleza barabara kutokana na
wingi wa magari (k.m. mpango wa dharura wa kukarabari barabara
uliobuniwa – URRP), na kwa ajili ya matengenezoya kawaida, uwezo
mdogo wa tasnia ya ujenzi, na ushiriki mdogo wa sekta binafsi.
Hata
hivyo Serikali imerazinisha na kuweka pamoja mfumo wa kitaasisi wa
kusimamia sekta ili kuleta ufanisi, utendaji utakiwao na
uwajibikaji. Wakala unaojitegemea, Wakala wa Barabara Tanzania,
(TANROADS), ulio na jukumu la kusimamia ujenzi wa barabara kuu,
ukarabati na matengenezo, umeanzishwa.
Bodi ya Taifa ya Babaraba yenye wakilishi kutoka
sekta binafsi, watumiaji na Serikali, husimamia shughuli za wakala
hii. Pia Serikali
imeanzisha Mfuko wa Babaraba ambao mapato yake makuu hutoka kwa
watumiaji wasioweza kukwepa ulipaji wake, kama chanzo kikuu cha
fedha za matengenezo ya barabara.
Serikali za Mitaa chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, ndiyo inayowajibika na barabara za Wilaya, za
Miji na za viungo zenye kuunganisha maeneo muhimu ya uzalishaji
kilimo vijijini, uchimbaji
mdogo mdogo wa madini, na utalii vijijini.
|