|
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Jamhuri ya umoja ambayo iko
chini ya demokrasia ya Bunge la vyama vingi vya siasa.
Mamlaka yote katika Jamhuri ya Muungano yanaendeshwa na
kudhibitiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kila Serikali ina nguzo tatu za utawala ambazo ni:
Serikali, Mahakama na Bunge.
Vyombo hivi vitatu vya utawala vina uwezo na madaraka ya
kusimamia shughuli zote za umma.
Aidha Mamlaka za Serikali za Mitaa huwa zinazisaidia
Serikali hizi kuu mbili katika shughuli zake za kutawala nchi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyo yenye mamlaka yote
yanayohusu shughuli za Muungnao pamoja na zile za Tanzania Bara
wakati ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mamlaka tu
kuhusu mambo ya Tanzania Visiwani ambayo hayako chini ya
makubaliano ya Muungano.
Serikali
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ndiye mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na
kamanda Mkuu a Majeshi. Viongozi ambao wako katika Mamlaka kuu ya Nchi ni Rais wa
Jamhuri, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Baraza
la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania.
Rais
ndiye kiongozi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Makamu wa
Rais ndiye msaidizi mkuu wa Rais kuhusu masuala yote ya Jamhuri ya
Muungano. Hususan
anamsaidia Rais katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila
siku za Muungano, kutekeleza kazi zozote atakazoagizwa na rais
pamoja na kuchukua madaraka ya Urais wakati Rais mhusika hayupo
madarakani au akiwa amesafiri kwenda nje ya nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungno ndiye Kiongozi mkuu wa
shughuli za Serikali Bungeni, na amepewa mamlaka ya kudhibiti na
kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano. Aidha
anatekeleza maagizo yoyote atakayopewa na Rais.
Rais wa Zanzibar ndiye kiongozi mkuu wa Serikali ya
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano, akiwemo Waziri
Mkuu, linateuliwa na Rais kutokana na Wabunge wa Bunge la
Muungano. Serikali
inatekeleza majukumu yake ya kila siku kupistia Wizara ambazo
zinaongozwa na Mawaziri. Kila
Wizara imepewa majukumu yake katika sekta mbalimbali.
Mahakama
Shughuli
za Mahakama Tanzania zinahusisha vyombo vitatu, ambavyo ni:
Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Mahakama Kuu za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, Tume ya Huduma
za Sheria Tanzania pamoja na mahakama za chini Tume ya Huduma za
Sheria Tanzania Bara in wajumbe watano, ambao ni:
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania (Mwenyekiti),
Jaji mmoja wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Tanzania, Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu na wajumbe wengine wawili wanaochaguliwa na Rais.
Mfumo
wa Sheria
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) katika utangulizi wake
inaeleza wazi kuwa wananchi wa Tanzania wameamua rasmi na kwa
dhati kujenga katika nchi yao jamii inayozingatia misingi ya
uhuru, haki, udugu na amani.
Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye
demokrasia ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe
waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi, na pia yenye mahakama
huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo
wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu
zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa
uaminifu.
Kwa
madhumuni haya basi, Katiba ya Jamhauri ya Muungano wa Tanzania,
1977, katika kifungu chake cha 4, inaeleza kwamba shughuli zote za
mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na
kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji
haki, na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na
kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.
Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; vyombo
vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya
Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungnao na Idara ya Mahakama
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya
kutunga Sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma
vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.
|