Uwekezaji

Katika jitihada za kuimarisha  mazingira ya uwekezaji  nchiniTanzania, Serikali hivi karibuni iliamua kupitia upya Sera ya Uwekezaji Tanzania ya February, 1990. Sera mpya ya Uwekezaji ilipitishwa na serikali mwezi Oktoba, 1996.

 

 Sera mpya ya uwekezaji inatilia mkazo mambo yafuatayo:

·        Uhasishaji na matumizi ya kiwango cha juu cha rasilimali za hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na nchi nyingine zinazoendelea na nchi zenye viwanda.

·        Kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi, ili kuendeza sekta ya biashara ya nje.

·        Kuhamasisha mitaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha juhudi za Taifa

·        Kuhimiza matumizi ya technolojia mpya katika shughuli mbalimbali hasa zile zenye uhusiano wa moja kwa moja na uongezaji tija, ubora na ushindani katika biashara.

¨      Kuongeza uwazi katika mfumo wa Sheria ambako kutasaidia kuinua na kulinda rasilimali zote zilizowekezwa

·        Kuondoa vikwazo vya kupata vibali vya kuwekeza nchini

·        Kuchambua wajibu za sekta binafsi ili kuipatia wajibu mkubwa zaidi

·        Kuoanisha taratibu za kiutawala na mfumo wa masoko kama njia ya kugawa rasilimali

·        Kuimarisha demokrasia ya vyama vyingi vya siasa .

·        Kuimarisha Utawala wa Sheria.

 

Dhamana ya Uwekezaji na Utatuzi wa Migogoro

 

Mali za wawekezaji nchini Tanzania zinalindwa na sheria dhidi ya utaifishaji na uporaji. Tanzani ni mwanachama wa Vyama viwili vya kimataifa vinavyoshughulikia migogoro ya mali za wawezekaji zilizotaifishwa ambavyo ni “International Centre for Investment Disputes” na “Multilateral Investiment Guarantee Agency” (MIGA).  Mgogoro wowote kati ya serikali na wawekezaji lazima kwanza usuluhishwe kwa kutumia majadiliano au kupeleka kwa usuluhishi katika vyombo vilivyotajwa hapo juu..

 

Uhamishaji wa Mitaji na Faida

 

Sheria zinaruhusu bila masharti kupitia Benki yeyote iliyoruhusiwa kuhamisha faida, kulipa madeni ya nchi za nje, ada, mrahaba au malipo yoyote yanayohusiana na teknolojia kutoka nje ya nchi, na malipo ya mishahara na mafao mengine ya wafanyakazi wa mataifa mengine wanaofanya kazi Tanzania.

 

Mikataba ya Uhamishaji wa Teknolojia

 

Hakuna vikwazo kwa makampuni kuhamisha teknolojia. Lakini kila Mkataba wa kuhamisha Teknolojia lazima usajiliwe na kituo cha Kusimamia Uwekezaji mara baada y a kukamilika.

 

Upatikanaji wa Mikopo  kwa Wawekezaji Wageni Kutoka Taasisi mbalimbali za Kitanzania

 

Kampuni yoyote inayofanya kazi Tanzania inaweza kupata mkopo kutoka Taasisi za Fedha za hapa nchini kwa mujibu wa viwango wilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania.

 

Sheria na Taratibu za Ajira

 

Tafadhali wasiliana na:

 

Idara ya Kazi Makao Makuu

Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana na Michezo

S.L.P. 9014

Dar es Salaam

 

Simu:    255 – 022 2110218/2110219

Fax:      255 – 022 2112045

 

Mtu wa kuwasiliana naye:            Kamishna wa Kazi

 

Sheria muhimu kuhusu ajira ni kama zifuatazo

 

Kima cha chini cha Mshahara

Mwongozo kwa Wawekezaji

 

Nyanja za uwekezaji zinazopatikana Tanzania Bara zimegawanywa katika sehemu  mbili muhimu:

 

Sekta Kuu

 

Uchimbaji madini, miundombinu (ujenzi wa barabara, madaraja, viwanja vya ndege, uzalishaji wa umeme, njia za mawasiliano ya simu, huduma za maji, na huduma nyingine za kusaidia uchimbani wa madini) na usafirishaji wa mazao na huduma nje yz nchi.

 

Sekta zinazopewa kimbaumbele

 

Kilimo ikiwa ni pamoja na ufugaji, usafiri wa ndege, majengo ya biashara, Benki za Biashara, Kusafirisha bidhaa nje ya nchi, Maendeleo ya Nguvu kazi, Viwanda,  mali asili ikiwa ni pamoja na uvuvi,  ukarabati na upanuzi, Utangazaji wa Redio na Televisheni, Utalii na Safari za Kitalii

Motisha Kwa Wawekezaji

Tanzania inatoa motisha kwa wawekezaji waliochagua kuwekeza hapa nchini. Motisha  hizi zimekusudiwa

 

§                     Kuwanufaisha wawekezaji kwa uamuzi wao wa kuwekeza hapa nchini

§                     Kuendana na mabadiliko ya mahitaji ya nchi

§                     Kuelekeza rasilimali katika mikondo inayohitajika sana kwa maendeleo ya kiuchumi

§                     Kupunguza pengo kati ya masikini na tajiri nchini

Motisha ya kodi kwa wenye vyeti vya kuwekeza vinavyotolewa na Kituo cha Uwekezaji na wawekezaji wengine

 

Sekta Kuu ( katika asilimia %)

Kituo Cha Uwekezaji Tanzania

 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania Na 26 ya mwaka 1997  kusimamia, kuratibu  na kusaidia  uwekezaji nchini. Kituo hiki ni muhimu kwa wawekezaji wote na kinafanya kazi ya mawasiliano kwa niaba ya wawekezaji kutoka hatua za hawali mpaka kukamilika  na kuanza kwa mradi unaokusudiwa.  Idara na Taasisi za serikali zinatakiwa kwa mujibu wa sheria kushirikiana na kikamilifu na kituo hiki katika kusaidia wawekezaji.

 

Kituo hiki kinashughulika na makampuni yenye mtaji usiopungua Dola za Kimarekani  laki tatu  (US $ 300,000) kwa yanayomilikiwa na wageni na dola za Kimarekani laki moja (US $ 100,000) yanayomilikiwa na wazawa. Makampuni yanayojishughulisha na uchimbani wa madini na biashara ya mafuta ya petroli, yanatakiwa kufuta taratibu za kupata vibali kama ilivyo katika sheria zinazohusika. Hata hivyo, kituo cha uwekezaji kinaweza kuwasaidia wawekezaji wote katika kupata  ruhusa na vibali vinavyohitajika chini ya sheria nyinginezo kuanzisha shughuli za uwekezaji nchini.

 

Shughuli za Kituo cha Uwekezaji

 

Kituo kinajishughulisha na

 

Ø               Kuanzisha na kusaidia hatua zinazoweza kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini kwa wawekezaji wa hapa nchini na nchi nzuri

Ø               Kutafuta, kukusanya, kuchanganua na kusambaza taarifa kuhusu nafasi za uwekezaji na njia za kupata mitaji ya kuwekeza, na kuwashauri wawekezaji, endapo wataomba, juu ya upatikanaji, uteuzi, au uzuri wa washirika katika miradi ya pamoja.

Ø               Kuanisha maeneo ya kuwekeza, mashamba, au ardhi na vilivyomo, mashamba au ardhi kwa ajili ya wawekezaji na uwekezaji kwa jumla.

Ø               Kuwasaidia wawekezaji wote, pamoja na wale ambao hawabanywi na Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania ya mwaka 1997, kupata vibali vyote muhimu, leseni na idhini, ruhusa, usajili na mambo mengine yanayohitajika kwa mujibu wa sheria ili mtu aweze kuanzisha shuguli za uwekezaji, na kuviwezesha vyeti vinavyotolewa na Kituo cha Uwekezaji kufanya kazi kikamilifu.

Ø               Kutoa, kuendeleza, kujenga kurekebisha,  kubadilisha, kutunza na kusimamia maeneo ya kuwekeza, mashamba au ardhi na zana zilizopo katika maeneo, mashamba, ardhi na kwa mujibu wa sheria  zinazohusika, kuanzisha na kusimamia kanda za kushulikia uuzaji wa bidhaa nje ya nchi.

Ø               Kutoa na kusambaza taarifa mpya kila zinapopatikana kuhusu faida au motisha zilizopo kwa wawekezaji

Ø               Kuandaa na kusadia shughuli za kuinua wawekezaji wa hapa wazawa ambazo ni muhimu katika kuwatia moyo  na kuongeza wawekezaji wazawa pamoja na mipango ya kuanzisha makampuni ya biashara.

 

Msaada wa Kuanzisha Makampuni

 

Kituo kitasaidia wawekezaji kuanzisha makampuni au kuyasajili kwa kufuata hatua zituatazo

 

q                Kuanzisha au kusajili kampuni

q                Kujaza fomu za kodi

q                Kujaza fomu za usajili wa kuwekeza na uhamiaji

q                Kumsaida mwekezaji  kupata leseni, vibali, nyenzo au huduma anazohitaji katika shughuli zake za kuwekeza.Endapo makabrasha yote muhimu yatawasilishwa kituoni kama yanavyotakiwa, kituo kinaweza kukamilisha taratibu za maombi katika siku kumi na nne.

 

Sheria za Uwekezaji

Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997

 

Wawekezaji, wote, wazawa na wageni ambao wana Cheti cha Motisha kinachotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania chini ya Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, wana haki ya kufaidika na vifungu vya Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 1973, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la thamani ya mwaka 1997 na  Sheria ya Ushuru wa Forodha ya mwaka 1976.

 

Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973

 

Katika  kuhesabu mapato na faida katika biashara zao wenye vyeti vya motisha wanasamehewa  asilimia mia moja (100%) ya gharama za mtaji iliyotumika katika mwaka wowote wa mapato. Endapo mahesabu ya kipato cha jumla yataonyesha nakisi (upungufu) kwa mwaka wowote wa mapato, kiasi hicho cha nakisi kitasamehewa kutoka katika mahesabu ya kipato cha muhusika kwa mwaka unaofuata wa mapato.

 

Kwa sekta ya madini, wawekezaji hawahitaji cheti cha motisha kupata msamaha uliotajwa hapo juu.  Aidha wawekezaji katika sekta hii wana motisha nyingine ya posho ya mtaji ya asilimia kumi na tano (15%). Posho hii inatolewa kwa salio la fidia ya matumizi ya mtaji ambayo yanafanya sehemu ya nakisi ya mwaka uliopita na iliyoruhusiwa kama punguzo kwa muhusika mwanzoni mwa mwaka wa mapato.

 

Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Mwaka 1976

 

Wenye vyeti vye motisha na ambao wamewekeza kwenye sekta zilizopewa kipaumbele kwa madhumuni ya kuimua sekta ya uwekezaji, kufuata na kifungu cha nne cha Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, watatozwa ushuru wa forodha wanapoingiza zana za mitaji kwa kiwango cha asilimia tano (5%).

 

Wanaowekeza katika sekta za miundombinu ya kiuchumi (ikiwa pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja, reli, viwanja vya ndege, uzalishaji wa umeme, mawasiliano ya simu, huduma za maji na nyinginezo zinazofanana na hizo) na katika sekta ya kanda ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi,  hawatatozwa ushuru wanapoingiza zana za mitaji kutoka nje ya nchi.

 

Wawekezaji wanajishughulisha na madini ambao hawajaanza uzalishaji wa kibiashara, wana haki ya kuingiza nchini bila kulipa ushuru aina zote za baruti, mafuta, vifaa vya viwanda na mahitaji mengine, mashine, magari, na vifaa vingine kwa matumizi ya shughuli za uchimbaji na utafutaji madini tu. Endapo watakuwa wamekwisha anza shughuli za Kibiashara, watalipa ushuru wa forodha kwa kiwango kisichozidi asili mia tano (5%).

 

Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Mwaka 1997

 

Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa uingizaji nchini wa zana za kuzalishia mali, unaofanywa na wafanyabiashara waliosajiliwa, inaahirishwa na itahesabiwa katika mapato watakapoanza uzalishaji wa kibiashara.

Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Mwaka 1976

 

Wakati wa ujenzi makampuni yaliyoruhusiwa wanasamehewa kulipa ushuru wa forodha na uingizaji bidhaa na kodi nyingine zinazofanana na hizo kwa kuingiza mashine, vipuri, mali ghafi, mafuta, magari na vifaa vingine  na ambavyo vitatumika kwa mradi wa ujenzi.

 

Mali ghafi kwa shughuli za majaribio pamoja na zana nyingine zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ambao ni muhimu kwa matumizi ya wataalamu wa kigeni vitasamehemewa kodi ya uingizaji bidhaa.

 

Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973

 

Katika  kuhesabu jumla ya mapato, unatolewa msamaha wa asilimia ishirini na tano (25%) ya jumla matumizi ya mtaji. Makampuni ambayo  yataonyesha yao ya kutaka kuwekeza zaidi huko  kutokana na faida itayopatikana katika miaka mitatu ya mwanzo baada ya kupata kibali cha kuwekeza huko Zanzibar, faida hiyo inayotaka kuwekezwa tena itasamehemewa kodi ya mapato ya Kampuni. 

 

 

Title

.

Title

.

Title

.