WEBSITE YA TANZANIA

Juhudi za kuanzisha website ya Taifa zilianza tangu mwaka 1996. Mradi huu ulitokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alimuagiza Waziri ya Fedha kufuatilia suala hilo. Wizara ya Fedha ilielekeza Benki Kuu ya Tanzania kutoa fedha kwa ajili ya maandalizi ya awali ya website hiyo. 

Benki Kuu iliitisha tenda ya kimataifa, na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknologia (COSTECH) ikishirikiana na Mtandao wa Habari na Teknolojia wa Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Ajili ya Maendelelo (COMNET – IT) waliteuliwa kufanya kazi hiyo.

Baadaye Benki Kuu iliona kuwa kazi hiyo ilikuwa inachukua muda mrefu mno; na kwa kuwa kazi hiyo ingekuwa ni jukumu la Serikali, hivyo iliomba Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kuchukua jukumu hili la kuanzisha na kuendeleza website ya Taifa.Website hii ilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin W. Mkapa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru tarehe 09.12.2001 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  Kwa kubonyeza tufe katika komputa (Soma tamko)

Malengo ya Website ya Tanzania
Lengo la kuanzisha website ya Taifa ni kudumisha na kuieleza taswira ya Tanzania ili ionekane na kufahamika kwa wananchi wake na ulimwengu mzima kwa madhumuni ya:-
  • Utawala bora.
  • Kuvutia uwekezaji.
  • Kuwezesha ushirikishwaji madhubuti katika utandawazi wa uchumi.

    Kwa upande wa Serikali website ya Taifa:
  • Itawezesha upatikanaji kwa urahisi wa habari za kiserikali katika mtandao wa intaneti.
  • Itaondoa marudio, utata na migongano ya habari za kiserikali katika mtando wa intaneti.
  • Itaweka utaratibu, mwafaka wa kuchapisha kwa njia ya intaneti.
  • Itatimiza malengo ya uwazi na ukweli.

Muundo wa Website ya Taifa

  • Kamati ya Taifa ya Kuendesha Website.
  • Timu ya Kitaifa ya Ufundi wa Website.
  • Kitengo cha Uratibu wa Website ya Taifa.

Mawasiliano:

Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji
S.L.P 9242
Dar es Salaam, Tanzania
Simu na Faksi: +255-22-2115083
Baruapepe: tnwinfo@plancom.go.tz