Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuMichezo

Michezo  ya riadha ya jadi ni michezo maarufu ya zamani kabisa kwenye jamii nyingi za Tanzania kabla ya kuja kwa wageni. Kuja kwa wageni na wakoloni nchini kuliingiza michezo mipya kama vile kandanda, hoki, mpira wa pete na ngumi.  Michezo ya riadha imerudi tena na kuimarishwa kwa viwango vya kisasa vya Kimataifa. Hata hivyo, kandanda ni maarufu na mchezo unaopendwa na watu wengi nchini ukifuatiwa na mpira wa kikapu, mpira wa pete na riadha.

Mara tu baada ya uhuru Serikali mpya ya Tanganyika ilitangaza nia yake ya kufufua, kuimarisha na kuendeleza vipengele vyote vya utamaduni ikiwemo michezo.  Mwaka 1962, Serikali iliunda Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana iliyopewa dhamana ya jukumu la kuhimiza michezo na kuanzishwa  mfumo utakaotimiza matarajio ya Taifa.

Mwaka 1967 Bunge lilitunga Sheria Na.12 ya mwaka 1967 iliyoanzisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lililopewa dhamana ya kusimamia na kuratibu michezo kwa kushirikiana na vyama vya Michezo vya Taifa.  Ili kufanya michezo iwe kwa wote, michezo kwa watu maalum ilihimizwa na kuwawezesha kushiriki kwenye mashindano ya Taifa na Kimataifa.  Michezo kwa watu wenye ulemavu wa mwili inajumuisha viziwi, wenye matatizo ya akili na vipofu. Hata hivyo, mpira wa miguu kwa wanawake unajikusanyia umaarufu zaidi na wachezaji mpira wa miguu wanawake wa Tanzania tayari wanashiriki kwenye mashindano ndani na nje ya Tanzania.

Kuna vilabu vya kandanda viwili maarufu jijini Dar es Salaam, Simba na Yanga vilivyoanzishwa tangu miaka ya 1930. Timu mbili hizi zina mashabiki na wapenzi wengi.

 

Mpira wa Pete Tanzania Mpira wa Miguu Tanzania
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-13 17:41:30
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page