Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuMuziki

Muziki una nafasi muhimu sana kwa takribani kila kabila na jamii duniani, na kusema kweli ni tabia ya binadamu.  Mataifa hueleza hisia zao kwa kutumia muziki. Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa muziki na kila kabila linaendeleza aina ya muziki wake.  Muziki ni miongoni mwa vipengele muhimu vya mila na utamaduni wetu.

Muziki nchini Tanzania ni wa aina mbalimbali kama vile muziki wa taarabu, dansi na muziki wa injili na umepiga hatua kubwa kama ilivyodhihirishwa na kuibuka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa ambavyo hukusanya mashabiki wengi mno.  Wasanii wengi wa Tanzania wamezalisha hazina kubwa ya kazi zao za ubora wa hali ya juu.

Wakati wa miaka ya mwanzo ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, muziki kama vile Ngoma umetumika kuhamasisha msaada na kuungwa mkono kwa harakati za ukombozi, kutangaza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea mfano mzuri ni mwanamuziki maarufu Mbaraka Mwaruka Mwinshehe na Bendi ya Moro, walikuwa na nyimbo zilizohimiza vijiji vya ujamaa na wengine walikuwa Marijani Rajabu, Cuban Marimba na wengine.

Licha ya kuwa zana ya harakati za ukombozi, muziki umewanufaisha vijana wengi kutokana na mtindo mpya unaojulikana kama Bongo Flava. Wamefungua fursa kubwa ya ajira katika uhandisi wa sauti na uchanganyaji, nafasi mbalimbali za uelekezaji, uongozaji na utengenezaji uandikaji “script”, taa, kamera na kujenga majukwaa.  Bongo Flava imewaletea umashuhuri na maendeleo ya wastani kwa vijana wengi wa Tanzania. Kutokana na mapato wanayopata, wameweza kujenga nyumba na kusaidia ndugu, jamaa na wazazi.

Muziki wa Dansi Muziki wa Taarabu
Muziki wa Bongo Flava
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-18 09:53:50
Kufaa
4.5
2 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page