Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasiliano

Umuhimu wa Sekta ya Mawasiliano kwa mwezeshaji wa maendeleo ya uchumi ya haraka kwa Tanzania dhahiri. Sekta hiyo inatoa mchango muhimu sana katika kuwezesha ssekta nyingine za uchumi kwa kutoa miundombinu ya mawasiliano ya huduma ili kuruhusu utiririko wa habari ya haraka, kubadilishana na kushirikiana miongoni mwa wateja kwa ajili ya kuongeza ufanisi kuimarisha utendaji na tija. Ulegezaji masharti katika sekta hii ulio katika hatua kubwa kuanzia huduma za mawasiliano kutoka kwenye sehemu hii.

Huduma zake nyingi zinatolewa na sekta binafsi na kutokana na gharama kubwa zinazohitajika katika kuanzisha shughuli, umilikaji mkubwa ni wa kigeni ingawa kuna sehemu nyingine ambazo washiriki wazalendo wanamiliki hisa. Sekta ya mawasiliano inasimamiwa na Sera ya Mawasiliano ya Simu (1997), Sera ya TEHAMA (2003), Sera ya Utangazaji Habari (2004) na sera ya posta (2003). Sekta hii inasimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) wa chombo kilichoanzishwa na sheria ya usimamizi wa udhibiti wa mawasiliano Tanzania(2003). Sekta ndogo zote ( mawasiliano ya simu, posta, usafirishaji,vifurushi, habari na tekinilojia za mawasiliano, huduma zinazojumuisha utangazaji) hivi sasa zinahesabiwa kuwa ni sekta moja kutokana na kushirikiana  tekinolojia, huduma na kanuni.

Kuanzishwa kwa TEHAMA nchini Tanzania kumewezesha ukuaji wa haraka wa huduma za mawasiliano. Huduma za TEHAMA hivi sasa zinafika kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini kupitia vituo mbalimbali ya shughuli nyingi za simu kwa jamii/taarifa mbalimbali. Hadi sasa kuna vituo 12 nchini kote vilivyopo mtuwetu (mtwara), kinamponda (singida), mpwapwa (Dodoma), Isaka (Shinyanga), Nchuchuma (Mtwara), Sengerema (Mwanza), Chuo cha Ualimu Kasulu (Kigoma), Ngara UNHCR (Kagera) na Rungwe (Mbeya) . kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia.

Tanzania ina masharti ya kisheria ya kikatiba inayoeleza vipengele mbalimbali vya tasnia ya vyombo vya habari. Katiba inahakikisha kuwepo kwa vyombo vya habari huru visivyoingiliwa. Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa 1) bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazo kupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayohaki na uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano (2) kila raia ana haki ya kupashwa habari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenye umuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwa jamii. Kwa maelezo zaidi tembelea Idara ya Habari (Maelezo).

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Posta
Mtandao Utafiti na Maendeleo
Mawasiliano ya Simu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Utangazaji Magazeti
Mawasiliano ya mtandaoni
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-26 08:20:18
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page