Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuPichaZiara za Kitaifa

Ziara za kitaifa ndiyo njia ya hali ya juu ya mawasiliano ya kidiplomasia kati ya mataifa na hufanywa kwa shamrashamra kubwa na itifaki ya kidiplomasia. Kutokana na uhusiano mzuri na nchi nyingine za kigeni. Tanzania inapata ziara nyingi rasmi za viongozi wa nchi za kigeni kutoka nchi nyingine mialiko rasmi nchini Tanzania inayohusisha Sherehe  za makaribisho zenye kukagua gwaride la heshima, magwaride na kupigwa kwa nyimbo za taifa na bendi ya polisi.

Mizinga 21 kupigwa kwa heshima ya viongozi wakuu wa nchi na 19 hupigwa kwa heshima ya viongozi wa kigeni wa Serikali. Kupeana zawadi kati ya kiongozi mkuu wa nchi ya kigeni na kiongozi mkuu wa nchi mwenyeji wa ziara hiyo, Dhifa za kitaifa hufanywa na mkuu wa nchi, na kiongozi mkuu wa nchi ya kigeni anakuwa mgeni rasmi. Mgeni huyo pia huandaliwa kutembelea maeneo muhimu kama vile kuweka shada la matamasha ya utamaduni huziunganisha nchi mbili, ambayo hufanyika kwa pamoja wakati wa ziara ya kitaifa.

Kiongozi mkuu wa taifa mara nyingi huambatana na mawaziri waandamizi wa serikali mara nyingi waziri wa mambo ya nje. Katika itifaki ya kidiplomasia, kuna ujumbe wa taasisi za kibiashara nao pia husafiri na kiongozi wa taifa wa nchi ya kigeni, hutoa fursa ya kuwasiliana na kukuza uhusiano wa kiuchumi, kijamii na kitamaduni na viongozi wa viwanda katika nchi inayotembelewa. Mwisho wa ziara ya kitaifa, kiongozi mkuu wa taifa ambaye ni mgeni kwa kawaida hutoa mwaliko mwingine ili katika siku zijazo mwenyeji naye afanye  ziara nchini kwake

Rais wa Marekani Barack Obama aitembelea Tanzania 2013 Ziara ya Rais wa China Xi Jiping nchini Tanzania Machi 2013
Ziara ya Waziri Mkuu wa Thailand Tanzania 2013 Ziara ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda nchini Tanzania 2014.
Ziara ya Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao nchini Tanzania 2014
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-17 20:01:48
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page