Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kilichoanzishwa nchini Tanzania kwa Sheria ya Bunge Na. 71 ya mwaka 1962 ni Shirika la Hiari na Huru la kusaidia Binadamu na limepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mahususi ya hiari ya kibinadamu wakati wa maafa dharura na wakati wa amani kama chombo cha kuisaidia Serikali. Chama hiki na sehemu ya mtandao wa duniani wa Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu tangu mwaka 1963 wakati ilipotekeleza masharti ya uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC).
Huduma na afua zilizotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania zinazingatia hatari na mazingira hatarishi nchini, zimelenga vikundi vingi hatarishi wakiwemo watoto, wanawake na wagonjwa wenye maradhi sugu, hasa watu wanaoishi na VVU / UKIMWI , Mayatima na Wazee na waathirika wa maafa/dharura.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-25 16:54:44