Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjeWashirika wa MaendeleoSEKRETARIETI YA MSAADA WA BAJETI WA JUMLA

Msaada wa bajeti wa jumla (GBS) ni mfuko unaotoa nyenzo kwa ajili ya kusaidia kupunguza umaskini nchini Tanzania.   GBS inatoa bajeti isiyo na masharti kwa Tanzania kwa kutumia mfumo wa tathmini wa pamoja na mchakato wa mazungumzo ya pamoja.  Miongozni mwa malengo ya msaada wa bajeti ni kuongeza kiwango cha nyenzo/rasilimali za hadhari zilizopo kwa Serikali.

Msaada wa bajeti ulianza kufanyakazi nchini Tanzania mwaka 2001, badala ya mfuko wa madeni ya kimataifa (MDF).  Kutokana na  uanzishwaji wake kumekuwa na ongezeko la hisia ya umiliki wa mchakato wa maendeleo wa Serikali pamoja na michango mikubwa iliyofanywa katika mchakato wa ufungamanishaji/upangaji na uwianishaji wa wahisani.  Aidha umeisaidia kuelekeza mazungumzo kuhusu masuala ya kimkakati na usimamizi wa kiuchumi na kutokana na hali hiyo, umeleta michango inayofaa katika kutunga sera (Tathmini ya pamoja ya msaada wa bajeti wa jumla, Tanzania, 1995-2004, Aprili 2005:143-144).

Msaada wa Bajeti wa jumla unapelekwa na  wahisani kwenye nchi kama Tanzania zenye utulivu wa kisiasa, zilizofanikisha programu za marekebisho ya kiuchumi, zilizoanzisha programu za marekebisho ya utawala na zilizoonyesha dhamira ya dhati ya kupunguza umaskini na malengo yaliyowekwa katika malengo ya maendeleo ya milenia (MDG).  Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa GBS duniani .  Kwa maelekezo zaidi kuhusu GBS nchini Tanzania  tembelea tovuti ya DPG Tanzania.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-30 15:21:12
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page