Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuPichaKumbukumbu ya Mashujaa

Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo  Julai 25 ya kila mwaka. Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa madhehebu ya dini, gwaride maalum la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Shughuli nyingine ni  uwekaji wa silaha za jadi ngao na mkuki na uwekaji wa maua  zoezi ambalo hufanywa na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia viongozi wengine walioteuliwa wakiwemo viongozi wa wazee, mabalozi, mkuu wa Majeshi na Mameya. Pia Siku ya Mashujaa huambatana na viongozi wakuu wa nchi kutembela maeneo ya kumbukumbu ya historia na makaburi walimozikwa mashujaa na wapigania uhuru wa Tanzania pamoja na ujumbe wa kuwahakikishia watanzania amani na Utulivu na usalama wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Kumbukumbu ya Mashujaa 2013 Kumbukumbu ya Mashujaa 2012
Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa 2011 Kumbukumbu ya Mashujaa 2014
Kumbukumbu ya Mashujaa 2015
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2016-01-01 18:48:36
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page