Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMisitu

Misitu na mapori ni miongoni mwa maliasili muhimu sana ambazo nchi imejaaliwa kuwa nazo. Nchi ina maeneo makubwa sana ya kufuga nyuki, yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 138,000 zinazokadiriwa kuwa katika eneo la hekta milioni 33.5 au kiasi cha 38% ya jumla ya eneo la ardhi . Sehemu ya eneo hilo, hekta milioni 13.5 zimetangazwa katika gazeti la Serikali kuwa ni misitu ya hifadhi ya taifa; ambapo hekta miloni 1.6 zinasimamiwa kama misitu ya vyanzo vya maji na hekta 90,000, hekta 150,000 na hekta 120,000 zinasimamiwa na serikali, viwanda binafsi na maeneo ya mapori ya viwango vidogo, na mashamba ya misitu ya ukubwa wa kati yanayomilikiwa na wamiliki wadogowadogo, kwa mfuatano huo. Nyingine zinasimamiwa kama misitu ya hifadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kuna misitu ya akiba ya taifa 600 na misitu ya akiba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa 200. Kwa sasa jumla ya hekta milioni 2.1 za misitu ziko chini ya usimamizi wa misitu wa jamii (CBFM) na hekta milioni 4.2 zimetangazwa kwenye gazeti la Serikali kuwa ni misitu ya akiba ya vijiji. Aidha, nchi ina maeneo makubwa sana ya kufuga nyuki, yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka. Hata hivyo ni tani 4,860 za asali na 324 za nta tu ndizo zinazozalishwa kwa mwaka au wastani wa 3.5% ya uwezo.

Serikali iko makini kushughulikia changamoto katika usimamizi wa maliasili na rasilimali za utamaduni nchini. Juhudi za pamoja zitafanywa kuimarishwa uhifadhi, ulinzi na usimamizi wa urithi huu wa asili/maumbile. Katika sehemu hii utapata taarifa za kina kuhusu maendeleo ya sekta ya misitu, sera, sheria  na shughuli zinazochangia  ukuaji wa pato la Taifa.

Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Tanzania Forest Service (TFS) Agency
Mfuko wa Misitu Tanzania
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2016-02-11 05:54:53
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page