Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMipango ya MaendeleoMfuko wa Maendeleo ya Jamii

Serikali imeandaa sera na mikakati mingi kuhusu kupunguza umaskini. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Umaskini na Kukuza Uchumi Tanzania (MKUKUTA) ulioanza mwaka 2000. Mkakati huo umeiwezesha Serikali kupata mafanikio makubwa yakiwemo kuongeza  kuenea kwa huduma za elimu na afya, uwekezaji katika miundo mbinu na kusaidia maendeleo ya kilimo.

Hata hivyo theluthi moja ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji ya msingi. Watu wanaoishi katika umaskini wanahangaikia kuzipa familia zao  vitu wanavyohitaji. Hawawezi kuwekeza katika mbegu bora au mbolea ili kuongeza chakula kwa familia zao wanachotakiwa kula,  na kwa hiyo wana fursa ndogo sana ya kupata ajira ambayo ingeweza kuwasaidia kupata fedha za kutosha kununulia chakula na mahitaji mengine muhimu na kuwa vigumu kumudu huduma za afya za msingi na wanashindwa kufuata utaratibu wa kuwapeleka watoto kliniki mara kwa mara.

Hali hii inaonesha haja ya kuwa na afua zinazolenga mahususi katika kupunguza umaskini na kupata uhakika wenye tija utakaowasaidia kuwalinda maskini dhidi ya athari za moja kwa moja za umaskini, kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya chakula na kuzuia hasara isiyokwisha ya rasilimali;  pia kuwezesha kaya zilizoathiriwa na umaskini kuwekeza kwa ajili ya baadaye na kuboresha maisha yao kwa muda mrefu.

Kwa hiyo Serikali imeanzisha TASAF III kama mojawapo ya programu za kushughulikia kupunguza umaskini. TASAF III ilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete  mwezi Agosti 2012.

Lengo la Uendelezaji wa Mradi Sehemu za Mradi
Walengwa wa Mpango Misingi ya Utekelezaji
Sera za Utekelezaji Major Focus of TASAF III
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2016-01-07 08:26:24
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page