Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuWasifu wa TanzaniaJiografia

Mahali

Tanzania iko Afrika Mashariki katika longitudo 290 na 410 Mashariki na latitudo 10 na 120 Kusini.

Eneo:Kilomita za mraba 945,000
Nchi Kavu:Kilomita za mraba 881,000
Zanzibar:Kilomita za mraba 2000
Maji:Kilomita za mraba 62,000
Misitu:3,350
Maji:Kilomita za mraba 62,000
Misitu:3,350

Sura ya Nchi

Tanzania ni nchi ya 31 kwa ukubwa duniani. Ikilinganishwa na nchi za Afrika. Tanzania ni ndogo kwa Misri na inakaribiana na ukubwa wa Nigeria. Hata hivyo Tanzania ni nchi kubwa katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi na  Rwanda.  Tanzania ina mandhari ya kuvutia katika maeneo makuu matatu ya sura ya nchi ambayo ni visiwa, mwambao upande wa mashariki na uwanda wa bara na milima.

Bonde kuu la ufa linalopita kuanzia kaskazini mashariki ya Afrika hadi kaskazini ya Tanzania ni alama nyingine inayoongeza mandhari nzuri ya nchi. Bonde la Ufa linaendelea hadi kusini ya Tanzania katikati ya  Ziwa Nyasa; tawi moja la bonde hilo linaelekea  Ziwa Nyasa hadi Msumbiji; na tawi jengine liko Kaskazini magharibi kupitia Rwanda  Burundi, Tanzania na upande wa magharibi wa Uganda. Bonde hilo lina maziwa  kama vile Rukwa, Tanganyika, Nyasa,  Kitangiri, Eyasi na Manyara.  Nyanda za Juu Kusini zinajumuisha  pamoja na  Kipengere, Udzungwa, Matogoro, Livingstone na uwanda wa Ufipa . Nyanda za Juu Kaskazini  zinajumuisha  Usambara,  Upare, Meru, Kilimanjaro,  Kreta ya Ngorongoro  na Oldonyo Lengai. Kutoka kwenye nyanda hizi za juu na uwanda wa kati kuna mfumo wa mtiririko wa maji kuelekea kwenye Bahari ya Hindi, Mediterania, Atlantiki na mfumo wa mtirirko wa maji ndani ya nchi.

Tanzania ina milima kwa upande wa Kaskazini Mashariki ikiwemo Mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu zaidi Afrika. Upande wa kaskazini na magharibi kuna maziwa makuu  ambayo ni Victoria ( Ziwa kubwa barani Afrika), Tanganyika ( Ziwa lenye kina kirefu zaidi barani Afrika lililomaarufu kwa  aina safi ya samaki) na upande wa kusini magharibi liko Ziwa Nyasa.

Hali ya Hewa Bio-anuai
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-07 16:07:58
Kufaa
5.0
2 Jumla
Inafaa Sana 2
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
2 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page