Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuWasifu wa TanzaniaUchumi

Tangu nusu ya pili ya miaka ya 1980, uamuzi mbalimbali umefanywa kufanya marekebisho ya uchumi na kurudisha mipango ya uchumi katika mwelekeo unaotarajiwa. Uchumi umerekebishwa kutoka umiliki wa umma hadi umiliki binafsi. Sekta binafsi imekuwa ndio mhimili wa ukuaji na hatua zinachukuliwa kuimarisha dhima na ushiriki wake. Ubia wa sekta ya umma na binafsi unatambuliwa kuwa ni kipengele muhimu katika kuhimiza ukuaji na maendeleo.

Kwa muongo mzima sasa, Tanzania imekuwa na ukuaji uchumi ulio thabiti. Ukuaji wa pato la taifa umekuwa wa kuvutia na kufikia wastani wa asilimia 6.6. kwa kipindi cha miaka mitano ( 2004-2008) ukuaji ulifikia asilimia 7.1. Hata hivyo kutokana na kudorora kwa uchumi duniani, mwaka 2009 ukuaji ulipungua hadi asilimia 5. Mwaka huu hadi June 2012 uchumi umerudia hali yake na kufikia asilimia 6.8. Ukuaji wa uchumi unategemea sana sekta za kilimo, utalii, uvuvi, misitu, ufugaji nyuki, uchimbaji madini, viwanda na nishati.

Kilimo: Kilimo kina mchango mkubwa na muhimu katika ukuaji wa uchumi. Kinaajiri 75% ya wananchi. Ufugaji unafanyika katika maeneo yenye mvua chache na ambayo hayana mbung’o. Mazao makuu ya biashara  ni kama kahawa, pamba, chai, mkonge, korosho, nazi, karafuu, tumbaku, mauwa, matunda na mboga.

Utalii: Vivutio vya utalii vya Tanzania ni pamoja na visiwa vya  Zanzibar vinavyojulikana kwa marashi yake na mahali pa starehe katika bahari ya Hindi; Mlima Kilimanjaro ulio mrefu kabisa  barani Afrika wenye kilele cha theruji ingawa upo karibu na Ikweta; Bonde la  Olduvai Gorge ambalo ni chimbuko la historia ya binadamu; Kreta ya Ngorongoro ambayo ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia; hifadhi ya Serengeti inayofahamika duniani kwa wingi wa aina ya wanyama na nyumbu wanaohama ambao haujawahi kuonekana duniani kote; Hifadhi ya wanyama pori ya Selous ambayo ni hifadhi kubwa  barani Afrika; Ziwa Tanganyika  lenye kina kirefu zaidi barani Afrika; na Ziwa Viktoria ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika. Vitu hivi vyote ilivyojaliwa Tanzania vinatoa fursa kwa burudani na uwekezaji katika hoteli, kambi, michezo ya kwenye maji, uwindaji na shughuli za uendeshaji utalii.

Uvuvi: Bahari ya Hindi na Ziwa Tanganyika vimethibitisha kuwa na samaki wengi na hivyo kuchochea uvuvi wa ndani, wakati Ziwa Viktoria ni chanzo cha Sangara ambao minofu yake inauzwa nchi za nje.

Misitu na Ufugaji Nyuki: Ardhi ya misitu isiyokuwa ya hifadhi (kilomita za mraba 1,903.8) ambayo ni misitu/ mapori yenye hifadhi ya taifa ( kilomita  za mraba 200) na misitu ya akiba iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali ( kilomita za mraba 1,251.7 ).

Uchimbaji wa Madini: Uchimbaji umevutia sana makampuni ya kimataifa kuwekeza kiasi kikubwa katika utafiti na uchimbaji wa dhahabu, madini ya chuma, almasi na tanzanite, gesi, chuma, makaa ya mawe, magadi soda, chumvi, vito na fosifati. Makampuni kutoka, Australia, Afrika ya Kusini na  Kanada na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha dhahabu kwa wingi barani Afrika.

Nishati: Tanzania inavyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, maji, taka na miamba. Serikali inahimiza upanuzi wa sekta hii. Hii ni sehemu ya sera ya Serikali inayohimiza uzalishaji wa nishati za ndani badala ya uagizaji wa bidhaa za petroli kutoka nje.

Uwekezaji: Serikali ya Tanzania imekusudia kuvutia uwekezaji wa nje kwa kuunda sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 kuwa ni sehemu ya mchakato huo. Jitihada hizo zimesababishwa kuundwa kwa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kinachobainisha fursa za uwekezaji na kusaidia wawekezaji kutatua vikwazo vyovyote vya uwekezaji vinavyoweza kutokea. Na pia Tanzania ilianzisha soko lake la hisa mwaka 1998 linaloitwa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

Biashara: Kahawa ni zao kuu linalouzwa nchi za nje, wakati mkonge na chai pia huingiza kiasi kikubwa cha fedha za kigeni. Bidhaa zilizotengenezwa, pamba, korosho, madini, maua na bidhaa za tumbaku huuzwa nchi za nje hasa India, Uingereza, Ujerumani, Japani, Uholanzi na Ubelgiji. Nchi inaagiza bidhaa kama vile bidhaa za matumizi, mitambo na mashine, vifaa vya usafirishaji, mafuta yasiyosafishwa na mali ghafi za viwandani. Bidhaa hizi zinaagizwa kutoka Afrika ya Kusini, Japani, Marekani, China na nchi nyinginezo. Tanzania ina ushirikiano wa biashara na nchi za jumuiya za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (EAC, SADC,COMESA). Tanzania pia inauza bidhaa zake kupitia  mikataba ya soko nafuu ya AGOA kwa Marekani, EBA kwa Jumuiya ya Ulaya, FOCAC kwa China, TICAD kwa Japani na Indo – Afrika  Partnership kwa India.


No Uchumi Faili / Anuani Miliki
1 Tanzania Zanzibar Socio-economic Profile 2014 5.6 MB
2 Tanzania Mainland Socio-economic Profile 2014 7.0 MB
3 National Socio-economic Profile 2014 7.5 MB
4 Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi 2014 31.3 MB
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-07 18:28:16
Kufaa
5.0
3 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.7
3 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page