Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuWasifu wa TanzaniaSiasa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha mfumo wa siasa ya chama kimoja kuanzia katikati ya miaka 1970 hadi 1992 uliporudishwa mfumo wa vyama vingi. Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, wa pili ulifanyika 2000, watatu ulifanyika 2005 na uchaguzi wa nne wa vyama vingi uliofanyika Oktoba 2010 ambao ulimrudisha madarakani kwa kipindi cha pili Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais wa Tanzania na Wabunge wanachaguliwa pamoja kwa wingi wa kura kutumikia kipindi cha miaka mitano. Rais anamteua Waziri Mkuu miongoni mwa wabunge walichaguliwa  kuwa msimamizi wa shughuli za Serikali Bungeni. Rais pia anateua  Baraza la Mawaziri. Katiba inampa mamlaka Rais kuteua wabunge kumi  ambao wanaweza kuingia katika Baraza la Mawaziri. Bunge pia linazingatia haki za wanawake kwa kutenga viti 75  vya wabunge wa kuteuliwa miongoni mwa vyama vya siasa kutokana na matokeo ya uchaguzi.

Bunge la taifa lililochaguliwa 2010 lina wabunge 320. Wabunge hawa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wabunge watano waliochaguliwa kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Viti Maalumu vya Wananwake ambao ni asilimia 30 ya wabunge ambao chama kimewapata,  wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi  Bara na 50 kutoka Zanzibar.  Aidha kuna wabunge  10  walioteuliwa na Rais. Kwa sasa chama cha mapinduzi kina asilimia 75 ya viti vya bunge. Sheria zinazopitishwa Bunge zinatumika Zanzibar kwa maeneo maalumu ya masuala ya muungano tu.

Baraza la Wawakilishi lina mamlaka ya kisheria kwa masuala yote  yasiyo ya muungano. Kuna Wawakilishi 76 katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambao ni pamoja na 50 waliochaguliwa na wananchi, 10 walioteuliwa na Rais wa Zanzibar, 5 kutokana na nyadhifa zao na mwanasheria mkuu. Mwezi May 2002, Serikali iliongeza idadi ya viti maalumu kwa wanawake kutoka 10 hadi 15 na kufanya idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa 81. Ni  dhahiri kwamba  Baraza la Wawakilishi la Zanzibar linaweza kutunga sheria za Zanzibar bila ya idhini ya Serikali ya Muungano alimradi sheria hizo hazitahusu masuala ya muungano.  Muda wa kuwa madarakani kwa Rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano pia.

Vyama vya Siasa vilivyopata Usajili kamili hadi Oktoba 2010

No.

Jina la Chama

1.

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

2.

Civic United Front (CUF)

3

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

4.

The Union for Multiparty Democracy (UMD) of Tanzania

5.

NCCR – Mageuzi

6.

National League for Democracy (NLD)

7.

Demokrasia Makini (MAKINI)

8.

United People’s Democratic Party (UPDP)

9.

National Reconstruction Alliance (NRA)

10.

Democratic Party (DP)

11.

Tanzania Democratic Alliance (TADEA)

12.

Tanzania Labour Party (TLP)

13.

The United Democratic Party (UDP)

14.

Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA)

15.

Progressive Party of Tanzania (PPT- MAENDELEO)

16.

Sauti ya Umma (SAU)

17.

Jahazi Asilia (JAHAZI ASILIA)

18.

Alliance for Tanzanian Farmers Party (AFP)

Chanzo: NBS (2010)

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-07 20:01:48
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page