Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuUtamaduniMichoro na Fasihi

Sanaa ya michoro huwasilishwa kama mapambo kwenye vifaa kama vile vyombo vya ufinyanzi, vifaa vya kusuka (vikapu), mikeka na mazulia na vitu vingine vya matumizi ya kila siku kama vile mitungi ya maji, kapu, visu na zana nyingine. Zaidi ya thamani ya matumizi ya vitu hivi na zana, vinatiwa mapambo ili yavutie.

Sanaa hii inazidi hujipatia umaarufu nchini Tanzania, imeongeza fursa za ajira kwa idadi kubwa ya Watanzania,  hasa vijana wanaojihusisha na sanaa. Michoro ya Tingatinga ni maarufu duniani kote kutokana na mitindo yao ya sanaa inayojulikana kuwa ni “Tingatinga”, jina lililokuwa la mwasisi wa mtindo huo, Edward Saidi Tingatinga aliyefariki kabla ya kufaidi  matunda ya sanaa yake.

Hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali ya Tanzania  kukuza sanaa, ikiwemo kuanzishwa kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa sheria Nam.23 ya mwaka 1984. BASATA kwa kushirikiana na wadau wengine imewezesha miradi mingi kwa lengo la kukuza sanaa.

Kwa upande wa fasihi, kwa kutumia aina mbili-ya kubuni na isiyo ya kubuni na mitindo miwili ya mathari na ushairi. Sanaa ya uandishi inakuwa , kuna vitabu vingi vya fasihi ya Kiswahili, kuandika kazi za fasihi pamoja na vitabu vingine kwa kitaaluma ni kipengele muhimu cha utamaduni. Kazi ya kwanza ya fasihi andishi ilikua ni utenzi wa Ras/’Ghuli wa mgeni Faqih wa Bagamoyo  mwaka 1853. Kazi nyingineya fasihi , maarufu kwa urefu wake katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara ni Bwana Nyombereke na Bibi Bugonoka, Ntulanalwo na Buliwhali cha Anicety Kitereza.

Waandishi wengine wa riwaya na tamthiliya  walijitolea miaka ya 1960 na 1970,  waliwaelimisha na kuwaburudisha wasomaji kwa miaka mingi wakati wakati huo huo kukuza kizazi kipya cha waandishi wa vitabu na wasanii. Baadhi ya waandishi hawa ni Shaaban Robert, Saadan Abdu Kandoro, Gabriel Ruhumbika, Euphrase Kezilahabi, Penina Mhando, Amanidina Lihamba, Elieshi Lema, Severin Ndunguru, Ebrahim Hussein, William Mkufya na Elvis Musiba.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-08 09:07:04
Kufaa
3.0
1 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page