Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuAlama za TaifaBendera ya Taifa

Tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri mpya ya Tanzania. Jina “Tanzania ” lilianza kutumika tarehe 29 Oktoba 1964. Kama lilivyo jina la nchi, bendera mpya ilikuwa muunganiko wa sehemu zilizounda nchi. Mstari wa chini wa rangi ya kijani uliokuwa wa bendera ya Tanganyika imechukua rangi ya bluu ya bendera ya Zanzibar, na mistari hiyo ilipangwa kiulalo ili kuipa hadhi sawa.

Maelezo  ya rangi:

Kijani 361c
Njano 116c
Bluu 299c

Kusema kweli hizi ni rangi zenye viwango isipokuwa rangi ya bluu, ambayo ni nyepesi kuliko rangi ya bluu ya “kawaida” lakini haikupauka kama ilivyo “bluu bahari”. Uwiano wa urefu na upana: tatu kwa mbili, kama 3’ x 2’, 6’ x 4’, 12’ x 8’

Maelezo:

Kijani- Njano- Nyeusi na bluu, yenye mstari wakati mweusi uliyowekwa katikati, ulalo unainukia kwenye mlingoti wa bendera hadi kwenye ukingo wa juu wa bendera, mistari miwili midogo ya njano inayogawanya sehemu ya juu ya pembetatu ambayo ni kijani na sehemu ya pembetatu ya chini ambayo ni bluu.

Uwiano wa rangi:

Mstari mweusi wa kati, uko katikati kwenye ulalo wa bendera wa 6’ x 4’, ni 13/18 ya bendera na upana(kumbuka futi 4 = inchi 48 ). Mistari ya njano ni 1/16 ya bendera na upana wa 3”Namba ya rangi na umuhimu wake: B.5(kwa mujibu wa kiwango cha Rangi cha Uingereza ambacho hivi sasa hakitumiki) Na. 2660,1995

Nyeusi BS Na – 9 – 103 = watu
Kijani  BS Na. 0 – 010 – Ardhi
Bluu BS Na. 0 – 012 – Bahari inayotuunganishia
Njano BS Na 0 – 002- Utajiri wa Madini 

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2018-10-12 12:07:56
Kufaa
2.3
3 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page