Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuAlama za TaifaWimbo wa Taifa

Mungu Ibariki Afrika ni jina la wimbo wa taifa la Tanzania. Asili yake ni wimbo wa "Nkosi Sikelel'i Afrika" wa Afrika Kusini. Enoch Sontonga ndiye mtunzi wa Nkosi Sikelel'i Afrika mwaka 1897. Sehemu ya wimbo huu inatumika pia katika nyimbo za taifa za Afrika Kusini na Zambia. Na huko nyuma ulitumiwa kama wimbo wa taifa wa Zimbabwe.

 

Mungu ibariki Afrika
Wabariki viongozi wake
Hekima, umoja na amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake.

 

KIBWAGIZO

Ibariki, Afrika
Ibariki, Afrika
Tubariki, watoto wa Afrika.

 

Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na umoja
wake kwa waume na watoto
Mungu, ibariki
Tanzania, na watu wake.

 

KIBWAGIZO

Ibariki, Tanzania
Ibariki, Tanzania
Tubariki, Watoto wa Tanzania

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 06:00:00
Kufaa
4.0
4 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
3.0
5 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 2
Si Rahisi kabisa 1

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page