Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuAlama za TaifaNgao ya Taifa

Sura ya kati ya Ngao ya Taifa ni ngao ya mpiganaji yenye sehemu ya juu ya dhahabu na chini yake kuna bendera ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania; sehemu nyekundu ikifuatiwa na mistari ya mawimbi yenye rangi ya bluu na nyeupe.

Sehemu ya rangi ya dhahabu inawakilisha madini yaliyopo nchini; sehemu nyekundu iliyopo chini ya bendera inaonyesha udongo mwekundu wa Afrika; wakati mistari ya mawimbi inawakilisha bahari, maziwa, mwambao wa Tanzania.

Sura zilizojidhihirisha zaidi kwenye ngao ni miali ya mwenge unaowaka ambao unaonyesha uhuru, elimu na maarifa; Mkuki unaonyesha ulinzi wa uhuru; shoka na jembe vilivyopishana vinaonyesha zana zinazotumiwa na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza nchi yao.

Ngao imewekwa juu ya Mlima Kilimanjaro. Katika kila upande wa ngao hiyo kuna pembe ya ndovu iliyoshikwa upande wa kushoto na Mwanamme na upande wa kulia na mwanamke.  Kwenye miguu ya Mwanamme kuna kichaka cha karafuu na miguu ya mwanamke kuna kichaka cha pamba vinanvyoonyesha ushirikiano.

 Wito wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ni “Uhuru na Umoja

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 07:33:32
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page