Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjeUhusiano wa KimataifaSera ya Mambo ya Nje

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa na kutumia Sera ya Nchi za Nje inayozingatia zaidi diplomasia ya uchumi ili kupata maslahi ya msingi ya taifa kama nchi huru.  Sera yenyewe inajihusisha zaidi na kushiriki kwa ukamilifu katika uwanja wa kimataifa, kimsingi imezingatia zaidi utekelezaji wa malengo ya kiuchumi, wakati huo huo inalinda mafanikio yaliyopita na kuimarisha kanuni za msingi za sera ya nchi za nje iliyopo Tanzania.

Sera mpya ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina malengo makuu yafuatayo; Kupanga, Kukuza na Kulinda maslahi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia kwa ukamilifu na kwa uendelevu diplomasia ya kiuchumi, kuhakikisha kuwa uhusiano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mataifa mengine na taasisi za kimataifa unazingatia maslahi ya kiuchumi, kujenga uchumi wa kujitosheleza, kudumisha amani na usalama wa taifa pamoja na kusaidia jitihada za kikanda na kimataifa kwa ajiili ya kuhakikisha kuwapo na ulimwengu bora na wenye amani.  Kuharakisha utangamano wa kisiasa na kiuchumi na kijamii kwa kanda na kuweka mazingira muhimu yatakayoiwezesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki kwa ukamilifu katika majadiliano ya kikanda na kimataifa.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 09:53:50
Kufaa
3.3
3 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 1
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
3.0
2 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 1
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page