Ukuaji wa biashara ni wakati biashara inapoongezeka ukubwa. Ukubwa wa biashara unaweza kupimwa kwa mapato ya mauzo, idadi ya wafanyakazi, mtaji wa hisa (idadi ya hisa mara bei ya kila hisa); soko la hisa - mauzo ya biashara ya bidhaa fulani kama sehemu ya uwiano wa mauzo yote ya aina hiyo ya bidhaa. Asilimia 5 ya soko la hisa ina maanisha kuwa 1 kati ya 20 ya bidhaa zote zilizouzwa, zinauzwa na biashara hiyo na idadi ya maduka ya kuuzia. Biashara ama inakua yenyewe au utwaaji na uunganishaji.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-02 09:07:04