Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjeUhusiano wa KimataifaTanzania katika Umoja wa Mataifa

Tanzania imekuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa tarehe 14 Desemba 1961, hata hivyo haina budi kuzingatia kwamba Tanganyika ilikuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa tangu Desemba 14 1961 na Zanzibar ilikuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuanzia Desemba 16, 1963. Baada ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mnamo April 26, 1964, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliendelea kuwa mjumbe mmoja na kubadili jina lake kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 1 Novemba, 1964.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki katika vyombo vikuu vya Umoja wa Mataifa ikiwemo Mkutano Mkuu, Baraza la Usalama, Baraza la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC). Kwa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mjumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo Mpango wa Mazingira ya Umoja wa Mataifa (UNEP) 2004-2007, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) 2004-2007, Umoja wa Mawasiliano ya Simu ya Kimataifa (ITU) 2002-2006 na Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) 2002-2006.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewahi kuwa mjumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) 1976-1979, 1991-1994,  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) 1998-2000, Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa (GEF) 1996, Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) 1975-1978, 1987-1990, 1999-2000, Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), 1969-1971, 1979-1982, 1985-1988, 1991-1993, Mpango wa Makazi wa Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) 2001-2004, Shirika la Afya Duniani (WHO) 1975-1978, 1993-1996, Shirika la Usafiri wa Anga la Kimataifa (ICAO) 1977-1980, 1983-1995,  Umoja wa Posta Duniani (UPU) 1989-1999, Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Desemba 2003, Benki ya Ujenzi na Maendeleo la Kimataifa (IBRD) Machi 2004, Chama cha Maendeleo cha Kimataifa (IDA) Mei 2004, Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Machi 2004 na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) 1978-1980.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 10:40:36
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page