Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuFedha ya TanzaniaUtoaji wa Noti za Benki

Fedha inayotumika Tanzania ni shilingi; ambapo tangu Benki Kuu ya Tanzania ilipoanzishwa 1966 imetoa noti na sarafu mbalimbali. Kutokana na uamuzi wa kuvunja Bodi ya Fedha ya Afrika Mashariki (EACB) na kuanzisha Benki Kuu kwa Tanzania, Kenya na Uganda, sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 1965 ilipitishwa na bunge Desemba 1965 na Benki ilifunguliwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius K Nyerere tarehe 14 Juni, 1966.

Sheria hiyo imeipa mamlaka Benki Kuu ya Tanzania kufanya kazi zote zilizokuwa zikifanywa na EACB. Hata hivyo baada ya miezi 8 tangu kuzinduliwa kwa Benki Kuu, mwezi Februari 1967 Azimio la Arusha lilitangazwa na kutokana na Azimio hilo Benki Kuu ililazimika kubadilisha sera zake. Maelekezo mengi yaliyohusu sera za fedha zisizokuwa za moja kwa moja zilizotajwa ndani ya sheria hazikufaa tena, kwa sababu hakukuwa na mazingira ya aina ya huduma katika mfumo wa ushindani ambapo maelekezo yasiyo ya moja kwa moja hayakufanya kazi.

Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ilirekebishwa mwaka 1978 na kusababisha kuongezwa kwa majukumu zaidi ya maendeleo katika benki hiyo. Kama ilivyoelezwa katika marekebisho hayo, Benki ilianzisha mifuko minne maalumu ambayo ni The Rural Finance Fund, The Industrial Finance Fund, The Export Credit Guarantee Fund na The Capital and Interest Subsidy Fund. Mifuko hiyo iliundwa kwa ajili ya kukopesha fedha na kutoa dhamana kwa mabenki na taasisi zingine za fedha dhidi ya mikopo yao na maendeleo ya sekta maalum za uchumi zilizobainishwa.

Marekebisho hayo ya sheria pia yalihamisha jukumu la mipango ya fedha kutoka wizara yenye wajibu wa mipango kwenda benki: kwa hiyo benki ilipewa mamlaka ya kukagua na kusimamia mabenki na taasisi nyingine za fedha, jukumu ambalo hapo mwanzo lilikuwa halifanywi na benki hiyo.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 15:21:12
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page