Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
 • Mwl. Julius K. Nyerere
 • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuFedha ya TanzaniaSarafu za Kumbukumbu

Sarafu za kumbukumbu ni zile zinazotolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio au jambo maalumu. Sarafu nyingi za kumbukumbu duniani zilitolewa kuanzia miaka ya 1960 na kuendelea ingawa kuna mifano ya sarafu za kumbukumbu nyingi zilizotolewa miaka ya nyuma zaidi. Sarafu hizo zina umbo la pekee linaloonyesha tukio lililosababisha kutolewa kwa sarafu hiyo. Sarafu nyingi za kundi hili hutumiwa zaidi na wakusanyaji wa sarafu wa aina hiyo tu, ingawa baadhi ya nchi hutoa sarafu za kumbukumbu kwa matumizi ya kawaida.

Sarafu za kumbukumbu zifuatazo zimetolewa na Benki Kuu ya Tanzania tangu 1966:

 • Mfuko wa Wanyama Pori Duniani (World Wild Life Fund)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu zinazopatikana kwa thamani za 2000  za madini ya dhahabu, zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 100, 50 na 25.

 • Uhifadhi wa Wanyama Pori (Wild Life Conservation)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu zinazopatikana kwa thamani za 1500  za madini ya dhahabu, zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 50 na 25.

 • Mfuko wa Watoto (Save the Children Fund)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu kwa ajili ya Save the Children Trust Fund zinazopatikana kwa thamani za 2000 za madini ya dhahabu. Zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 100.

 • Muongo wa Umoja wa Mataifa kwa Wanawake (UN Decade for Women)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu kwa ajili ya UN Decade for Women zinazopatikana kwa thamani za 1000 za madini ya dhahabu. Zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 100.

 • Sarafu Maalum ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Special Coins)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu kama sarafu maalum ya Mwalimu Nyerere; zinazopatikana kwa thamani za 10 za madini ya dhahabu.

 • Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Uhuru wa Tanganyika (20th Anniversary of Tanganyika Independence)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya uhuru wa Tanganyika. Zinazopatikana kwa thamani za 2000 za madini ya dhahabu. Zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 200 na shilingi 20.

 • Kumbukumbu ya Miaka 24 ya Uhuru wa Tanganyika (20th Anniversary of Tanganyika Independence)

Hizi ni fedha za kumbukumbu zilizotengenezwa na Benki Kuu kuadhimisha kumbukumbuku ya miaka 24 ya uhuru wa Tanganyika. Zinazopatikana kwa thamani za 2500 za madini ya dhahabu. Zipo pia za madini ya fedha za thamani ya shilingi 250 na shilingi 25.

 • Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Benki Kuu ya Tanzania (20th Anniversary of Bank of Tanzania)

Sarafu hizi zimetengenezwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Benki Kuu ya Tanzania. Zinapatikana kwa madini ya fedha na shaba na nikeli kwa thamani ya shilingi 20.

 • Kumbukumbu ya Miaka 25 ya Benki Kuu ya Tanzania (20th Anniversary of Bank of Tanzania)

Sarafu hizi zimetengenezwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya Benki Kuu ya Tanzania. Zinapatikana kwa madini ya fedha kwa thamani ya shilingi 25.

 • Noti za benki zinazotumika

Benki Kuu ya Tanzania imeanzisha noti mpya za benki tangu januari 2011. Noti hizo mpya ni za thamani ya shilingi 500, 1000, 2000, 5000 na 10000.

Noti za benki za zamani zilizotolewa mwaka 2003 zinaendelea kutumika pamoja na toleo hili jipya. Fedha hizi zitaondolewa kwenye mzunguko polepole mpaka tarehe itakapotangazwa kuwa hazitumiki tena.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 16:54:44
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page