Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliBunge Kazi za Bunge

Katika kutekeleza kazi zake, Bunge linasaidiwa na Tume ya Huduma za Bunge, Kamati za Kudumu na Sekretarieti ya Bunge. Kazi kuu za Bunge ni kumhoji waziri yeyote kuhusu masuala ya umma yaliyo ndani ya dhamana yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kujadili utendaji wa kila wizara wakati wa kikao cha mwaka cha Bunge la Bajeti, kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaotakiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji sheria na kujadili na kuridhia mikataba na makubaliano ambayo Jamhuri ya Muungano ni mhusika na masharti yake yanahitaji idhini.

Aidha hutunga sheria zinazotumika kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia Bunge hutunga sheria zinazotumika Tanzania Bara tu; Zanzibar ina Baraza la Wawakilishi wake linalotunga sheria mahususi kwa Zanzibar (Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lina wajumbe 50, wanaochaguliwa kutumikia kwa kipindi cha miaka mitano).

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 20:48:34
Kufaa
4.5
2 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.5
2 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page