Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliBunge Wajibu wa Katibu wa Bunge

Katika kuliwezesha Bunge kutoa huduma kwa ufanisi na uhakika, Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inataka kuwapo kwa Katibu wa Bunge. Katibu huyo ambaye huteuliwa na Rais ndiye Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa shughuli za Ofisi ya Bunge zinatekelezwa kwa ufanisi kwa mujibu wa masharti ya Katiba na sheria nyingine zinazohusika.

Ibara ya 88 ya Katiba inataka kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Bunge yenye idadi ya maofisa watakaohakikisha ufanisi katika utekelezaji wa kazi za bunge na wabunge.

Jukumu kuu la Katibu wa Bunge ni kumshauri Spika na wabunge kuhusu Bunge, utaratibu na haki. Anamsaidia Spika kuandaa kila kikao cha Bunge na hukaa bungeni mwanzo wa kila kikao. Pia huandika uamuzi rasmi na kutoa ushauri kwa Spika au wabunge katika jambo linalohitaji utaratibu.

Katibu wa Bunge hushauri kuhusu mwenendo na taratibu za Bunge; kanuni rasmi na zisizo rasmi zinasimamia shughuli za kila siku bungeni. Jukumu la kumsaidia Katibu wa Bunge katika kufanikisha shughuli hizo ni la wafanyakazi wa idara zote za ofisi ya bunge, ambao hutumikia katika nyadhifa mbalimbali.  

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-12 11:27:22
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.0
1 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page