Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliBungeHistoria

Bunge la Tanzania liliasisiwa kabla ya Uhuru mwaka 1926 kama Baraza la Kutunga Sheria la Tanzania Bara, iliyojulikana kama Tanganyika. Bunge la kutunga Sheria liliundwa kwa mujibu wa amri ya Baraza la Tanganyika na sheria ilitungwa na Bunge la Uingereza. Sheria ilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali nchini Tanganyika tarehe 18 Juni 1926 na Baraza liliundwa Dar es Salaam tarehe 7 Desemba 1926 chini ya uenyekiti wa Gavana wa Tanganyika Sir Donald Cameron. Baraza hilo lilikuwa na wajumbe 20 wote walioteuliwa na Gavana. Miongoni mwa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Baraza la Kutunga Sheria yalifanywa mwaka 1953 wakati Spika wa kwanza alipoteuliwa kuchukua nafasi ya Gavana kama Mwenyekiti wa Baraza. Spika huyu wa kwanza alianza kazi tarehe 1 November 1953.

Mabadiliko makubwa ya pili yalikuwa mwaka 1958 wakati kwa mara ya kwanza Baraza lilikuwa na wajumbe wachache waliochaguliwa na wananchi. Hatua hii ilileta mabadiliko makubwa katika siasa za Tanganyika kwa sababu ulikuwa ni uchaguzi wa kwanza ulioruhusiwa katika koloni na ilikuwa ni mara ya kwanza kwa vyama vya siasa vilivyosajiliwa kushiriki katika uchaguzi. Vyama vitatu vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi huo ni Tanganyinga African Union (TANU), United Tanganyika Party (UTP) na African National Congress (ANC). Hata hivyo ni chama cha TANU tu ndicho kilichoshinda katika baadhi ya majimbo na kuwa chama cha kwanza  kuwa na wajumbe katika Baraza la Kutunga Sheria.

Mabadiliko makubwa ya pili kwenye Baraza la Kutunga Sheria yalitokea mwaka 1960 wakati uchaguzi wa pili wa Baraza ulipofanywa. Mabadiliko hayo yalikuwa sehemu ya matayarisho ya Uhuru wa Tanganyika. Kwa mara ya kwanza, wananchi waliwachagua wajumbe wote wa Baraza la Kutunga Sheria baada ya kuwatangua wajumbe wote walioteuliwa na Gavana. Jina la Baraza la kutunga Sheria lilibadilishwa na kuitwa Bunge. Mabadiliko haya yalikuwa muhimu kikatiba kwa sababu Malkia wa Uingereza au Mkuu wa Serikali ya Uingereza aliridhia.  Mabadiliko kwenye Bunge yalikuwa na maana kuwa baada ya uhuru, sheria zitakazotungwa hazitakwenda Uingereza kuridhiwa. Badala yake Rais wa Tanganyika huru ataridhia sheria zote. Tangu kufanyike mabadiliko ya jina la Bunge  kumekuwa na mabadiliko machache hasa kwenye idadi na aina ya wajumbe. Hata hivyo, dhima na mamlaka yamebaki kuwa yale yale.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-12 12:14:08
Kufaa
5.0
2 Jumla
Inafaa Sana 2
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
2 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page