Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjePasipoti Viambatisho vya Maombi ya Pasipoti

Maombi ya pasipoti yataambatanishwa na cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo ya kuzaliwa au cheti cha kuandikishwa uraia cha mwombaji (iwapo mwombaji ni raia wa kuandikishwa), cheti cha kuzaliwa, au hati ya kiapo ya kuzaliwa au cheti cha kuandikishwa uraia cha mzazi au wazazi wa mwombaji, picha ya pasipoti ya hivi karibuni, safi na isiyo kwenye fremukama itakavyoelekezwa na mamlaka ya utoaji na kwa mwombaji mwenye umri chini ya miaka 18, ridhaa ya maandishi ya wazazi au walezi wa kisheria.

Licha ya masharti yaliyoelezwa apo juu, mwombaji wa pasipoti atatakiwa  kuwasilisha nyaraka zifuatazo kutegemea aina ya safari inayokusudiwa:

I)Safari ya Binafsi

Maombi ya safari ya binafsi yataambatanishwa na uthibitisho wa shughuli za mwombaji, barua ya mwaliko, tiketi ya kwenda na kurudi, barua ya idhini ya mzazi au mlezi kwa mwombaji wa chini ya umri wa miaka 18, barua ya idhini ya mwajiri iwapo mwombaji ameajiriwa na barua kutoka kwa afisa mtendaji wa kata/sheha, anakoishi mwombaji.

II)Safari ya Kikazi

Maombi ya safari ya kikazi yataambatanishwa na ahadi ya ajira, tiketi ya kwenda na kurudi na barua kutoka kwa afisa mtendaji wa kata/sheha anakoishi mwombaji.

III)Safari ya Kimasomo

Maombi ya safari ya kimasomo yataambatanishwa na barua ya uadhili, vyeti vya masomo, barua ya udhamini, uthibitisho wa malipo ya udhamini binafsi, barua ya udhamini ya mwajiri iwapo mwombaji ameajiriwa na barua ya idhini ya mzazi au mlezi kwa mwombaji wa chini ya umri wa miaka 18.

IV)Safari ya Kidini

Maombi ya safari ya kidini yataambatanishwa na barua ya mwaliko na barua kutoka shirika la dini linalotambulika lililosajiliwa  na lenye kuhusika na safari hiyo.

V)Safari ya Matibabu.

Maombi ya safari ya matibabu yataambatanishwa na barua kutoka kwa mganga mkuu, au uthibitisho wa daktari aliyesajiliwa na barua ya idhini kutoka Wizara ya Afya.

VI)Safari ya Kimichezo

Maombi ya safari ya kimichezo itaambatanishwa na barua kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) au Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) au barua kutoka Chama cha Michezo kilichosajiliwa na barua ya mwaliko.

VII) Safari ya Maskauti

Maombi ya safari ya maskauti yataambatanishwa na barua kutoka Chama cha Maskauti kinachohusika, barua ya idhini kutoka kwa mzazi au mlezi  kwa mwombaji chini ya umri wa miaka 18.

VIII) Safari ya Kiserikali

Maombi ya safari ya kiserikali yataambatanishwa na barua ya mwajiri, barua ya mwaliko na kitambulisho cha mwombaji.

IX) Safari ya Kibiashara

Maombi ya safari ya kibiashara yataambatanishwa na leseni halali ya biashara na tiketi ya kwenda na kurudi.

X) Safari ya Kibaharia

Maombi ya safari ya kibaharia yataambatanishwa na mkataba wa ajira, kitabu cha safari za kibaharia, vyeti vya shule na barua kutoka kwa chama cha mabaharia kinachohusika.

Zingatia:

Hati ya kiapo inayohusu kuzaliwa kwa mwombaji itaelezwa au kuapwa na mzazi au mlezi wa kisheria au mtu aliyekuwepo mahali alipozaliwa mwombaji mwenye umri usiopungua miaka mitano au zaidi ya umri wa mwombaji au ndugu/ jamaa wa karibu wa mwombajialiyejua/kuarifiwa kuzaliwa kwa mwombajina wazazi. Wakati mwingine, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anaweza kumhitaji mwombaji wa pasipoti aonyeshe uthibitisho wa uraia wa wazazi wake.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-15 08:20:18
Kufaa
1.0
1 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
4.0
1 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page