Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMahakama

Nchini Tanzania mfumo wa Mahakama umeundwa na Mahakama za ngazi mbalimbali na haiingiliwi na Serikali.  Tanzania inafuata na kuheshimu kanuni za Katiba za utenganishaji wa Mamlaka.  Katiba inaruhusu kuanzishwa kwa Mahakama Huru, na kuheshimu kanuni za Utawala wa Sheria, Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu mfumo wa Mahakama Nchini Tanzania.  Mfumo wa Mahakama, Tanzania Bara (huanzia ngazi ya juu hadi chini) ikiwemo Mahakama ya Rufaa, Mahakamu Kuu ya Tanzania, Mahakama za Mahakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo.  Katika Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, watoa hukumu za kesi wanaitwa majaji.  Katika Mahakama nyingine zote wanaitwa Mahakimu.  Majaji wanateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania, Mahakimu 25  wanateuliwa moja kwa moja na Tume.  Pia katika sehemu hii utaona orodha ya kesi, amri za kila siku na hukumu na Sheria zilizotengwa.  Kwa maelezo zaidi tembelea Tovuti ya Mahakama Tanzania.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-15 13:00:54
Kufaa
4.3
4 Jumla
Inafaa Sana 2
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
3.8
4 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 1
Si Rahisi Sana 1
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page