Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMipango ya Maendeleo Dira 2025

Matayarisho ya Dira ya maendeleo Tanzania (TDV), 2025 yalianza mwaka 1994 na hatimaye serikali ilizindua Dira hiyo, mwaka 1999. Kiini cha Dira ya 2025 ni kwamba  ifikapo 2025, Tanzania itakuwa imepitia katika mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo ili kupata hali ya kipato cha kati, ikiwa na viwango vya juu vya viwanda, ushindani , maisha bora , utawala wa sheria na kuwa na jamii iliyoelimika na inayopenda kusoma. Kimsingi, Dira ya maendeleo Tanzania, 2025 imeeleza kwa muhtasari matarajio ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini katika robo ya kwanza ya karne ya 21 kwa lengo la kufikia hali ya kipato cha kati nchini (MIC), kwa kuwa na pato la kila mtu la Dola za Marekani 3,000 (kwa kulinganisha na kipato halisi) ifikapo mwaka 2025.

Dira ya 2025 ilipangwa kutekelezwa katika mfululizo wa mipango ya maendeleo ya miaka mitano mitano. Hata hivyo wakati Dira ya 2025 ilipoanza Tanzania ilikuwa inatekeleza sera na marekebisho ya kitaasisi magumu, chini ya nchi maskini zenye madeni makubwa (HIPC) ili iweze kukubaliwa katika mpango wa msamaha wa madeni, kwa kuzingatia hayo na kwa msaada wa wabia wa maendeleo, mikakati ya kupunguza umaskini (PRS) ya muda mfupi na muda wa kati ilianzishwa kama njia ya kupunguza tatizo, ambayo ilikuwa mfumo wa utekelezaji wa Dira kutokana na kutokuwepo kwa mpango wa kupunguza umaskini wa miaka mitatu (2000-2003), ukafuatiwa na mpango wa kwanza wa miaka mitano wa mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) 2005 2010). Ingawa MKUKUTA ulitayarishwa kama mkakati wa utekelezaji wenye matokeo makubwa, ulikosa vipaumbele vya masuala ya maendeleo na kuweka hatua mahususi za kimkakati kutimiza malengo ya Dira ya 2025.

 

Na.

Dira ya 2025

Ukubwa

1.

Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Tanzania (2011-2016)

2.6 MB

2.

Dira ya Maendeleo Tanzania 2025

3.0 MB

 


No Dira 2025 Faili / Anuani Miliki
1 Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011-2016 616.0 KB
2 Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 3.0 MB
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-15 14:34:26
Kufaa
4.3
3 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 2
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
3.3
3 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 2
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page