Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjeUshauri wa KusafiriViza

Wageni wote wanatakiwa kuwa na viza isipokuwa raia wa baadhi ya nchi za Afrika na Jumuiya ya Madola. Inashauriwa kupata viza mapema kutoka kwenye Balozi za Tanzania kwa kuwa baadhi ya mashirika ya ndege yanaweza kuhitaji viza kabla ya kupanda ndege. Hata hivyo unaweza kupewa viza wakati unapowasili katika viwanja vya kimataifa vya Dar-es-salaam, Zanzibar na Kilimanjaro na katika vituo vya mpaka wa Tanzania vya Namanga, Sirari, Horohoro,Tunduma na Taveta. Pasipoti ni lazima ziwe halali kwa angalau miezi sita.

Raia wa nchi zilizosamehewa masharti ya viza watapewa hati za wageni za kupita bila kikwazo katika vituo na maeneo ya kuingilia rasmi nchini.Wale wanaosafiri kwenda Zanzibar wanahitaji viza hata kwa safari ya siku moja. Masharti ya viza yanabadilika kila baada ya muda, kwa hiyo unashauriwa uhakikishe hali ya sasa mapema kabla ya kusafiri. Kwa maelezo zaidi kuhusu masharti ya viza, tafadhali tembelea Idara ya Uhamiaji Tanzania.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-16 14:34:26
Kufaa
5.0
3 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
2 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page