Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiSehemu za kutembelea

MAHALI PA KUTEMBELEA

Tanzania ni nchi yenye vitu vya kulinganisha na vyenye utukufu, barani Afrika ambavyo bado ni vya kiasili na havijavumbuliwa. Kuna kilele chenye theluji cha Mlima Kilimanjaro na fukwe zenye jua za Zanzibar, makundi makubwa ya wanyama wanaolisha kwenye Nyanda za Serengeti na Mlima Ol donyo Lengai, unaolipuka volcano polepole. Kutokana na utajiri mkubwa wa maliasili, bila shaka Tanzania ina kitu cha kumpa kila mtu.

Katika sehemu hii utaona maeneo kumi bora nchini Tanzania, yaliyoorodheshwa kwa umaarufu wao. Ukisoma, utaibua mambo mazuri ambayo Afrika haijawahi kukupa kustaajabu, kujaribu, changamoto, burudani, lakini orodha hii bado ni mwanzo tu. Wakati maeneo maarufu sana na yanayofahamika duniani kote ni vidokezo tu vinavyoketa watalii nchini kwetu ni mwanzo tu, kuna mambo mengi zaidi ya kuangalia kuliko watu wanavyofikiria. Katika mahali pa kutembelea tunaeleza maeneo yote muhimu na kujitahidi kadiri iwezekanavyo kukupa muhtasari wa mahali kote kunakovutia nchini kwetu, kuanzia magofu ya Waswahili ya kuvutia lakini yasiyofahamika sana kwenye mwambao wa Kusini hadi makabila ya wawindaji na wakusanyaji ya Nyanda za juu za Kaskazini. Utapata maelezo kuhusu maeneo ya safari za kutalii na hifadhi za Taifa na maeneo tengefu yatakayokusaidia kupanga ratiba ya safari zako, wakati sehemu ya Miji na Majiji kukupa taarifa muhimu na ya kuvutia yanayokidhi matakwa yako. Je hujaamini kuwa Tanzania ina kila kitu? Ukiangalia  Visiwa tu utaamini hayo. Mwisho, kama ungependa kuona baadhi ya maeneo ya asili maarufu sana Duniani, angalia milima na volcano au maziwa  kila unachotaka – kipo Tanzania. Panga Safari yako.

Ukiwa na mahali mbalimbali pa kutembelea na vitu vingi vya kuangalia kupanga safari yako nchini Tanzania kunahusisha utafiti wa makini na kufanya uamuzi mgumu. Wageni wengi wanaona kwamba safari moja haitoshi kutendea haki maeneo mengi ya kutembea nchini, na wanarudi tena na tena kufurahia maajabu ya wanyama pori, mandhari ya kuvutia na makaribisho ya ukarimu ya watu wake.

Hapa nchini tunaeleza kwa muhtasari baadhi ya jinsi ya  kufika Tanzania na jinsi ya kutembea hapa na pale mara tu unapofika Tanzania – kusafiri kwa barabara, kwa ndege, bahari na reli vyote vinatumika sana nan i njia zinazofaa. Maelekezo yetu ya Vitu unavyotakiwa kuleta yanajumuisha vitu visivyopatikana kwa urahisi Tanzania, na vitu ambavyo, ama uwe Safarini kuburudika kwenye fukwe zenye mwanga wa  jua, hutakiwi kuvikosa.

Mambo muhimu ya maelezo ya Safari kuorodhesha vitu vya kuzingatia kuhusu ubadilishaji wa fedha na upataji, kuzingatia afya yako unapokuwa safarini, tahadhari za malaria, bima ya safari, upataji huduma za hospitali na kliniki, viza na usalama. Kupanga Safari yako “itakueleza kila unachotaka kujua ili ujiandae ipasavyo kwa safari yako.

Hifadhi za Taifa Sehemu za Kihistoria
Utalii wa Kitamaduni Miji na majiji
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-22 15:21:12
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page