Utoaji wa elimu bora kwa Watanzania wote unapewa kipaumbele cha hali ya juu na Serikali ya Tanzania kwa sababu ya umuhimu wake katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa taifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaiona elimu kama kitu kimoja cha wazi na kinachoeleweka, kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu. Serikali inatambua kuwa elimu bora ni nguzo ya maendeleo ya taifa, kwa sababu ni kwa kutumia elimu ndipo taifa linapopata watumishi stadi wa kuhudumia sekta mbalimbali kwenye uchumi wa taifa.
Muundo wa Elimu Rasmi na Mfumo wa Mafunzo nchini Tanzania ni miaka 2 ya elimu ya awali/ chekechea, miaka 7 ya elimu ya Msingi, miaka mine ya Sekondari ya Kawaida na miaka miwili ya Sekondari ya Juu na miaka mitatu au zaidi ya Elimu ya Chuo. Mfumo wa Elimu hasa una ngazi tatu, ambazo ni:- Msingi, Sekondari na Chuo. Sehemu hii inakueleza kuhusu mpango wa maendeleo, mipango mkakati yake na ripoti. Unaweza kupakua kwa matumizi yako.