Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliWafanyakazi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa ajira ina nafasi kubwa sana katika kukuza ustawi wa taifa, kuondoa umasikini, ushirikishwaji wa jamii pamoja na kuimarisha amani na utulivu katika jamii. Kuwepo na fursa za kazi na kujiajiri ni muhimu katika kutimiza haki ya kufanya kazi  kama njia ya kuwa na ukuaji uchumi endelevu, uondoaji umaskini na ufikiaji wa malengo na ahadi za kitaifa na kimataifa ikiwemo Malengo ya Maendeleo ya Milenia.

Serikali pia imedhamiria kwa dhati kuweka mazingira bora kwa ajili ya uhimizaji wa ajira kamili na kazi nzuri. Kwa hivyo masuala ya ajira yamejumuishwa katika mkakati wakupunguza umasikini unaojulikana kama MKUKUTA. Aidha Tanzania imeridhia mikataba kumi ya msingi ya  Shirika la Kazi Duniani na tayari imeshapitia upya Sera ya Ajira ya Taifa kama sehemu ya jitihada hizi.

Zaidi ya hayo, Serikali imetunga  Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004 inayohakikisha haki za kazi za msingi na kuweka viwango vya ajira vya msingi. Sheria inatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya ubaguzi katika ajira yeyote  nakuwataka waajiri kuchukua hatua ya dhati ya kuhakikisha wanaume na wanawake wanapata malipo yaliyo sawa kwa kazi yenye thamani inayolingana.  Sheria nyingine ni pamoja na Sheria ya afya na usalama kazini, Sheria ya fidia kwa wafanyakazi na Sheria ya Ajira kwa Wenye Ulemavu  Na. 2 ya Mwaka 1982.

Pata taarifa zaidi kuhusu namna afua za Serikali zinazolenga kuwavutia na kuwabakisha kazini watumishi wenye sifa pamoja na kuwashawishi wafanyakazi kwa kushughulikia mishahara na malipo sawa katika ajira. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti za Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira, TAESA na Wizara ya Kazi na Ajira.

Haki za Watumishi Mafao ya Watumishi
Kanuni za Maadili Mafunzo
Nyaraka Ajira ya serikali
OPRAS Miundo ya Utumishi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 10:40:36
Kufaa
4.6
8 Jumla
Inafaa Sana 7
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.4
8 Jumla
Rahisi Sana 6
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 1

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page