Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na Usalama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa mfumo wa muundo wa Jeshi la Tanzania, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ina wajibu wa kuhakikisha kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasaidia na kulinda nchi dhidi ya maadui wote wa nje na kusaidia mamlaka ya raia na nguvu ya raia. JWTZ lilianzishwa mwaka 1964 baada ya maasi yaliyosababisha kuvunjwa kwa jeshi lililotokana na wakoloni, Tanganyika Rifles(TR). Rais Nyerere aliamua kujumuisha JWTZ kwenye mfumo wa siasa na kwenye jamii inayoitumikia. Maofisa wa kijeshi na viongozi wa kisiasa walibadilishana nyadhifa jeshini, kwenye chama na Serikali. JWTZ lilikua jeshi la ulinzi na miongoni mwa majeshi ya taifa yaliyosaidia harakati za ukombozi.  JWTZ imesaidia Sera za nchi za nje na ulinzi. Tanzania kwa kushirikiana kwenye harakati za ukombozi kusini mwa Afrika na mafunzo ya majeshi ya ukombozi katika ulinzi wa nchi kutokana na ukosefu wa usalama katika mipaka na Uganda na mpaka wa Msumbiji. Kusudio la kuanzishwa Jeshi la Mgambo lilikua kujenga dhana ya uwajibikaji na fahari ya nchi kwa wananchi kwa kuwakaribisha raia nao washiriki katika ulinzi wa nchi. Jeshi la kujenga Taifa (JKT) lilianzishwa ili kuwawezesha vijana wa Tanzania kujenga umoja wa kitaifa na kuhudumia nchi. JKT huwapa vijana mafunzo ya kijeshi na stadi za kujitegemea. Jeshi la Kujenga Taifa na Mgambo hulipa JWTZ jeshi la akiba kuongeza uwezo na nguvu za kijeshi.

Sehemu hii ina taarifa kuhusu mfumo wa ulinzi na wenye hadhi ya kijeshi ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Magereza, Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Sera ya ulinzi ya Taifa na Jeshi la Mgambo.       

Jeshi la Wananchi Tanzania - JWTZ Jeshi la Magereza
Sera ya Ulinzi ya Taifa Jeshi la Kujenga Taifa
Mgambo Jeshi la Polisi
Zimamoto na Uokoaji
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 14:34:26
Kufaa
4.6
5 Jumla
Inafaa Sana 4
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.3
4 Jumla
Rahisi Sana 3
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 1
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page