Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMipango ya MaendeleoArdhi

Dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ni kuwezesha  na kuweka mazingira mazuri na mfumo wezeshi kwa ajili ya kufanikisha lengo la kuwa na makazi endelevu yaliyo sawa, salama na yenye ulinzi, yenye afya na ufanisi nchini Tanzania. Ukuaji wa miji wa haraka uliofanyika katika miongo minne iliyopita, umeongeza na utaendelea kuongeza kiwango cha watu wanaoishi katika maeneo ya mijini.

Katika hali kama hiyo Serikali inakusudia kuwekeza katika utoaji wa kutosha wa nyumba na uendelezaji wa makazi endelevu nchini. Hii itafikiwa kwa kutumia kwa ukamilifu juhudi zilizopo na za baadaye na fursa katika utoaji wa nyumba na uwekezaji wa miundo mbinu, usimamizi na utengenezaji wa miundombinu hiyo. 

Hayo yanafanywa kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali na wadau katika sekta ya umma, binafsi na isiyo rasmi  na Asasi zisizo za Serikali (AZISE), kama vile UN-HABITAT na mashirika ya kijamii (CBO). Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu programu ya maendeleo ya ardhi, mpango wa kimkakati na ripoti. Unaweza kupakua kwa matumizi yako.

Mpango wa Uboreshaji wa Miji Huduma na Makazi Tanzania Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Miji na Makazi Tanzania
Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-05 17:41:30
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page