Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMakaziUendelezaji Miliki

Kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya nyumba na haja ya kuwafanya watanzania wamiliki nyumba, Serikali imelielekeza Shirika kupanua wigo wa utendaji wake. Hivi sasa Serikali inalitazamia Shirika, pamoja na mambo mengine, lijielekeze zaidi katika kuleta uwiano katika mihimili miwili ya miliki. Badala ya kujikita kwenye usimamizi wa miliki pekee, shirika pia liweke mkazo katika ujenzi wa miliki mpya. Kuwawezesha watu kumiliki nyumba hasa wakati huu ambapo sheria za mikopo ya nyumba na Hati Pacha zimepitishwa. Kujenga nyumba nyingi za gharama nafuu kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini na cha kati nchini. Kutumia mali zake (nyumba ambazo ziko sehemu zenye hadhi) ili kujiendesha kibiashara na kupunguza matatizo ya nyumba. Kushirikiana na wawekezaji binafsi katika kutekeleza miradi mikubwa huku likilinda maslahi ya umma.

Malengo ya kimkakati 

 • Kujenga nyumba zisizopungua elfu kumi (10,000) kwa ajili ya kuuza na kupangisha kwa wananchi
  wa kipato cha kati na kipato cha juu ifikapo mwezi Juni, 2015.
 • Kujenga nyumba zisizopungua elfu tano (5,000) kwa ajili ya kuuza na kupangisha kwa wananchi wa
  kipato cha chini ifikapo mwezi Juni, 2015.
 • Kutengeza majukumu ya mwendelezaji mkuu wa ardhi ifikapo mwezi Juni, 2013.
 • Kutafuta kiasi cha shilingi trillioni moja na nusu (1.5 trillioni) kwa ajili ya kutekeleza
  miradi mbalimbali ifikapo Januari, 2015.
 • Kuanza uuzaji wa nyumba zilizojengwa kwa ajili ya kuuza ifikapo mwezi Desemba, 2011.
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-10 09:53:50
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page