Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Vibali
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Kibali cha ukazi Daraja "C" kinaweza  kutolewa kwa wageni wanaokusudia kuingia na kuishi nchini Tanzania kwa madhumuni  zaidi ya yale yaliyobainishwa kwa ajili ya kupewa kibali cha ukazi Daraja “A” au “B” kama walivyo wanafunzi, watafiti, wafanyakazi wa kujitolea, watu wanaohudhuria kesi kwenye mahakama za sheria, watu waliokuwa wakazi na wanakaribia kuondoka nchini (kufunga shughuli zao) na watu wanaopata matibabu hospitalini.

Masharti:

 • Fomu za maombi (TF1) zilizojazwa nakala mbili kwa ukamilifu.
 • Mkataba wa usalama kwa jumla (TIF 13)
 • Wasifu wa mwajiriwa (CV)
 • Nakala ya pasipoti ya Taifa yenye muda wa kutumika usiopungua mwaka mmoja.
 • Nakala za vyeti vya elimu vilivyothibitishwa.
 • Barua za uthibitisho wa ajira kutoka kwa mwajiri wa zamani (kama yupo)
 • Picha sita za pasipoti

Utaratibu:

 • Nenda jaza fomu ya maombi katika ofisi ya uhamiaji
 • Toa taarifa baada ya idhini ya kibali.
 • Lipa ada iliyoelezwa ya Dola za marekani 500.
 • Idhini haitatumika baada ya siku 60 kuanzia tarehe ya taarifa
  hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 29 ya Kanuni za Uhamiaji ya mwaka 1997.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page