Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Maji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Huduma ya maji ni muhimu sana kwa maisha - tunatumia maji kwa kunywa, kunawa, kupikia na kumwagilia mimea. Bila maji mimea, wanyama na watu watakufa. Ugavi wa maji na upatikanaji wa maji hutolewa na taasisi za umma, mashirika ya biashara, juhudi za jamii au watu binafsi.

Taratibu:

  • Nenda kwenye ofisi ya ugavi wa maji iliyo karibu yako ukiwa na kitambulisho.
  • Jaza Fomu ya Maombi katika ofisi za ugavi wa maji kuomba kuunganishwa maji.
  • Ofisa wa kanda atapima eneo/majengo yako na kukupatia makisio ya gharama.
  • Mwombaji atarajie kuunganishiwa huduma ya maji katika kipindi cha siku 14 baada ya kukamilisha malipo ya ada /gharama ya kuunganishiwa maji
  • Kila mteja ahakikishe ameungiwa dira ya maji 
  • Ankara ya kwanza ya mteja itamfikia mwezi mmoja baada ya kuunganishiwa maji

Gharama za uunganishaji maji.

  • Gharama za vifaa
  • Uchimbaji na ufukiaji
  • Gharama za usimamizi

 

 

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page