Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imejumuisha utaratibu wa maombi ya mkopo kwa kutumia mfumo  wa maombi ya mkopo kwa mtandao (OLAS). Mfumo wa kutumia tovuti ni kwa waombaji wa mara ya kwanza na kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.

Masharti:

 • Namba ya shule/mtihani ya kidato cha nne ikiwemo mwaka aliofanya mtihani kama inavyoonekana kwenye cheti.
 • Maelezo ya udhamini kama vile jina kamili, kitambulisho, anuani ya posta, namba ya simu ya mkononi na barua pepe.
 • Namba ya utambulisho wa malipo inatakiwa

Taratibu:

 • Tembelea Mfumo wa Maombi ya Mkopo  kwa Mtandao
 • Soma maelekezo ya utoaji mkopo
 • Lipa ada ya maombi ya mkopo kwa njia ya mifumo ya malipo kwa simu ya mkononi
 • Jisajili katika OLAS
 • Jaza fomu ya maombi kwa mtandao
 • Chapa fomu zote za maombi
 • Ambatisha nyaraka zinazotakiwa kwenye maombi yako
 • Peleka fomu zote za maombi kwa uthibitisho wa hakimu au mthibitishaji rasmi/wakili wa mamlaka ya serikali za mitaa
 • Peleka fomu zote za maombi zilizokamilika kwa njia ya EMS kwa HESLB.

Zingatia:

 • Mtu yeyote ambaye wakati wa kujaza fomu ya maombi ya mkopo anajua kwamba anatoa taarifa  ya uongo, iwe kwa mdomo, kwa maandishi au kwa mtandao, kuhusu jambo lolote litakaloathiri maombi ya mkopo husika atakuwa na hatia ya
  kutenda kosa na atastahili kutozwa faini isiyopungua Tshs. 1,500,000/= au kifungo
  kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja.  (kifungu 23(1) ya Sheria ya HESLB Na.
  9 ya Mwaka 2004 kama ilivyorekebishwa).
 • Iwapo itabainika kuwa mkopo ulitolewa kutokana na taarifa za uongo zilizotolewa na
  mkopaji, bodi itabatilisha mkopo huo na mkopaji atashtakiwa.
 • Waombaji wanashauriwa kutunza stakabadhi ya EMS na nakala ya fomu zote za maombi
  ya mkopo kwa ajili ya marejeo ya baadae na ufuatiliaji.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page