Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kujiunga
OFISI INAYOHUSIKA
Soko la Hisa la Dar es Salaam

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Soko la Hisa ni jengo au mahali ambapo hisa na dhamana nyingine zinanunuliwa na kuuzwa; wanachama madalali na wafanyabiashara za hisa na dhamana wanaokutana na kufanya biashara kwa kufuata sheria na kanuni za soko hili.

Masharti:

 • Cheti cha kuandikishwa/usajili
 • Katiba na Hati ya kuhamishia mali kwa mdhamini
 • Katiba na kanuni za kampuni
 • Wasifu wa Wakurugenzi, ofisa maadili, ofisa utumishi/mwidhinishaji
 • Masijala na uthibitisho wa utaalamu wa  kiufundi unaotakiwa.
 • Leseni ya biashara, au usajili mwingine wowote wa kisheria au usimamizi kutoka mamlaka husika.
 • Mpango wa biashara
 • Dhamana za Benki na masharti mengine ya fedha.
 • Wasifu.
 • Nakala halisi za cheti cha mwenendo bora.

Taratibu:

 • Omba udahili kama mwanachama wa soko la hisa kwa maandishi.
 • Bainisha kundi la uanachama.
 • Wasilisha taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita au kipindi kifupi kadiri inavyokubalika kwa DSE.
 • Wasilisha tamko la kisheria la ofisa utumishi/mwidhinishaji.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page