Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kusajili
OFISI INAYOHUSIKA
Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Hizi ni kampuni zilizoandikishwa/kusajiliwa nje ya Tanzania. Ofisi zao nchini Tanzania zinahesabiwa kama matawi ya kampuni ya kigeni. Hata kama wachangiaji wote au wenye hisa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kampuni hizo zinahesabiwa kuwa ni za kigeni tu. Zinasajiliwa kwa mujibu wa Sehemu ya xii ya Sura ya 212.

Masharti:

  • Nakala za katiba na kanuni za kampuni zilizothibitishwa
  • Notisi ya mahali pa ofisi iliyosajiliwa katika nchi ya maskani
  • Orodha ya wakurugenzi wa kampuni
  • Wakazi wa nchini ambao ni wawakilishi wa kampuni

Taratibu:

  • Jaza fomu kwa makini na jitahidi kujibu maswali yote
  • Ambatisha nyaraka zote muhimu
  • Lipa dola za marekani 1,100 za ada ya usajili.
  • Wakati wa uwasilishaji hakikisha kuwa unaambatisha nakala ya stakabadhi ya malipo
  • Cheti cha uandikishwaji kampuni kinapewa waombaji

Zingatia:

  •  Malipo yote yanalipwa kwa Msajili wa Makampuni

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page