Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kujiunga
OFISI INAYOHUSIKA
Shirikisho la Hakimiliki

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

 

Mwandishi wa kitabu au wamiliki wengine wa hatimiliki anaweza kuomba uanachama wa COSOTA. Usajili wa wanachama na kazi zao hufanya kwa  mujibu wa kanuni za Hatimiliki na haki shiriki (usajili wa wanachama na kazi zao)  za mwaka 2005, notisi ya Serikali Na. 6 ya tarehe 20 Januari, 2006.

Masharti:

  • Nakala mbili za picha za pasipoti za mwombaji
  • Nakala ya kitambulisho cha kazi, pasipoti, kitambulisho cha taifa au cheti cha kuzaliwa cha mwombaji.
  • Nakala ya kitambulisho cha kazi , pasipoti, kitambulisho cha taifa au cheti cha kuzaliwa cha jamaa/ndugu wa karibu.
  • Majina ya wanakikundi na mwakilishi iwapo ni kikundi, bendi au kwaya.

Taratibu:

  • Lipia fomu ya maombi kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo.

Na. ya Fomu

ADA

JINA LA FOMU

FOMU YA KUKAMILISHWA

CST 4

5,000/=

Fomu ya maombi ya uanachama ya mtu mmoja mmoja

Mtu mmoja mmoja

CST 5

10,000/=

Fomu ya maombi ya uanachama ya kikundi

Kikundi cha Kampuni

CST 6

10,000/=

Mchango wa mwaka wa mwanachama mmoja mmoja

Ada ya Mwaka

CST 7

50,000/=

Mchango wa mwaka wa kikundi mwanachama

Ada ya Mwaka

CST8

HAKUNA

Kukabidhi kazi ya sanaa

Mwombaji

  • Jaza kwa ukamilifu fomu ya maombi kutoka COSOTA
  • Ambatisha nyaraka zote muhimu
  • Ambatisha nakala ya kazi yako halisi ya sanaa unayokusudia kuisajili.
  • Wasilisha fomu yako ya maombi kwenye ofisi ya COSOTA
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page